Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia Prof Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Rais wa Sudani Kusini Dkt Barnaba Marial Benjamin mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Na Mathias Canal, KILIMANJARO.
Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia Prof Adolf Mkenda (Mb)leo tarehe 20 Julai 2022 amempokea Waziri wa Mambo ya Rais wa Sudani Kusini Dkt. Barnaba Marial Benjamin katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Dkt Barnaba amewasili nchini kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Sudani Kusini Mhe Salva Kiir kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa nchi na serikali wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 21-22 Julai 2022 katika ukumbi Ukumbi wa kimataifa wa mikutano-AICC Jijini Arusha.
0 comments:
Post a Comment