Tuesday, 12 July 2022

KUHANI MWAKIBINGA : JITOKEZENI KWA WINGI KUHESABIWA SIKU YA SENSA

...
 

Kuhani Ayubu Mwakibinga

Na Derick Milton, Bariadi.

Kiongozi wa Kanisa la World Miracle Mission Central (WMCC) kutoka Mkoani Shinyanga Kuhani Ayubu Mwakibinga amewataka wahumini wa kanisa hilo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa na makazi.


Amesema kuwa zoezi hilo ambalo litafanyika Agosti 23, 2022 ni muhimu sana kwa nchi ambayo inataka kuwaletea watu wake maendeleo, ambapo ameeleza yeye atakuwa mstari wa mbele siku hiyo kwenda kuhesabiwa.


Kiongozi huyo wa Dini amesema hayo jana mjini Bariadi wakati wa mkutano wake wa injili uliofanyika mjini Bariadi na kuhudhuliwa na mamia ya wananchi wa mji wa Bariadi wakiwemo wahumini wake.


Alisema kuwa zoezi la sensa linatakiwa kuungwa mkono na kila mtanzania mpenda maendeleo, kwani serikali haiwezi kuleta miundombinu mbalimbali kwa wananchi bila ya kujua wako wangapi na wanahitaji nini.


Aliongeza kuwa watu wengi wamekuwa wakilalamikia serikali kwa kushindwa kuwaletea huduma za mbalimbali za kijamii, ambapo ameeleza ili serikali iweze kutimiza jukumu hilo lazima ijue ina watu wangapi.


Amewataka wahumini wake kila mmoja kuhakikisha anamwasisha mwezake kwenda kuhesabiwa Agosti 23, 2022, ili serikali iweze kuweka mipango yake ya kuwaletea watanzania maendeleo.


“ Agosti 23, 2022 ni siku ya sensa kitaifa, na sisi kama raia wa nchi hii, ambayo inaoongoza na mmama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan tunao wajibu wa kumuunga mkono Rais wetu kwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuhesabiwa, Mimi nitakuwa mstari wa mbele kuhesabiwa.” Alisema Kuhani Mwakibinga…..


“ Nchi lazima iwe na takwimu, tukipanga maendeleao tujue wako wangapi, tunaweka pale kulingana na takwimu na watu wako pale, tusipohesabiwa tutajua watu wako wangapi?....


Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa Dini amewataka wahumini wake kuendelea kumwombea Rais Samia kwani amekuwa kiongozi mwenye maono wa kuletea maendeleo kwa kasi wananchi wake.


“ Tumemwona Rais wetu kwa kipindi hiki kifupi amejenga shule, vituo vya Afya kwa wingi sana, tunao wajibu wa kumlinda kiongozi wetu kwa kumwombea na wale wenye nia mbaya na yeye” ,alisema Kuhani Mwakibinga

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger