Friday, 22 July 2022

CHAMA CHA MAPINDUZI WAFURAHIA UWEKEZAJI MKUBWA UNAOFANYWA NA SERIKALI KATIKA SEKTA YA ELIMU NCHINI

...

 


Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaridhishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 21,2022 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipotembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.

Kabla ya kutoa kauli hiyo Shaka alipata nafasi ya kutembelea mabanda mbalimbali yaliyokuwepo kwenye Maonesho hayo na kisha akatoa maelezo kuhusu na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini ukiwemo Wizara ya elimu na Taasisi zake.

"Katika elimu kuna uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ambao unaendelea kutoa matunda mazuri katika sekta hii na Chama chetu kinaridhishwa sana,"amesema Shaka na kuelezea hatua kwa hatua yanayoendelea kufanywa na Serikali ili kuendelea kuiboresha zaidi ya sekta ya elimu.

“Nimetembelea mabanda ya taasisi mbalimbali za elimu zinazoshiriki maonyesho haya, nimejionea na kusikia mambo makubwa ya maendeleo,” ameeema na kuongeza katika bajeti ya mwaka huu ongezeko la fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na wizara nzima ya elimu, ni hatua muhimu iliyotengeneza mazingira rafiki kwa sekta ya elimu,"amesema Shaka.

Akielezea zaidi Shaka amesema huko nyuma kulikuwa na malalamiko mengi aliyokuwa akiyapokea ofisini kwake kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, yaliyomlazimu kutembelea Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na sasa hali imeimarika.

Amefafanua kwamba Rais Samia amefanya kazi kubwa katika sekta ya elimu katika kipindi cha mwaka mmoja na moja ya mambo ambayo hayazungumzwi sana ni namna alivyosamehe deni la karibia Sh. trilioni 1.1 ambalo lilikuwa halilipiki kwa bodi hii ya mikopo.

Aidha Shaka amesema Sh.bilioni 985 ambazo zimetengwa katika bajeti ya 2022/2023 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya vikuu, kuwapatia mafunzo ya taaluma wahadhiri na kununua vitendea kazi itazidi kutengeneza mazingira mazuri kufundisha na kujifunzia.

“Azma na utayari wa Rais Samia kuibeba sekta hii ya elimu sote tumekuwa mashuhuda, name nataka niwaambie kuwa ameanza vizuri, tunaamini uboreshaji huu utaendelea."

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Charles Kihampa amesema wanaishukuru Serikali ya CCM kwa kuendelea kuitazama kwa karibu sekta ya elimu nchini na kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja madarakani, uwekezaji mkubwa umefanywa a na Rais Samia katika elimu.

Amesema uwekezaji huo umechochea ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa kwa ajili ya elimu ya juu kutoka wanafunzi 8,7934 hadi 100,620.Aidha Profesa Kihampa amemueleza Shaka kuhusu juhudi zinazoendelea katika kuboresha elimu na taaluma inayotolewa na Vyuo Vikuu nchini.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akieleza jambo kwa  Viongozi waandamizi wa  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania  (TCU), Prof Charles Kihampa  pamoja na Mkurugenzi Udahili na Menejimenti ya Data Dkt.Kokuberwa Mollel mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kutembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR-MMG
.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipokewa na Viongozi waandamizi wa  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania  (TCU), Prof Charles Kihampa  pamoja na Mkurugenzi Udahili na Menejimenti ya Data Dkt.Kokuberwa Mollel wakati akiwasili leo Julai 21,2022 katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kutembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza mbele ya waandishi wa vyombo vya habari mara baada ya kutembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  leo Julai 21,2022mkoani Dar es Salaam.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akisaini kitau cha wageni katika moja ya banda la chuo kikuu cha Mzumbe,wakati akiendelea kutembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  leo Julai 21,2022 mkoani Dar es Salaam.Pichani kati ni Katibu Mtendaji wa TCU Prof Charles Kihampa na kushoto ni Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Bi. Rose Joseph

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania  (TCU), Prof Charles Kihampa alipotembelea kwenye moja ya banda la Wakala wa Masuala ya elimu kutoka nchini India,wakati akitembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo Julai 21,2022 mkoani Dar es Salaam


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger