Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack akizungumza na baadhi ya watumishi wa MSD (hawapo picha) mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha Makorora kilichopo mkoani Tanga
Vifaa tiba kwaajili ya upasuaji vilivyopo katika kituo cha afya Makorora mkoani Tanga vikiwa tayari kwaajili ya kutoa huduma ya upasuaji. Vifaa hivyo vimekabidhiwa hivi karibuni na Bohari ya Dawa (MSD). Vifaa tiba kwaajili ya upasuaji vilivyopo katika kituo cha afya Makorora mkoani Tanga vikiwa tayari kwaajili ya kutoa huduma ya upasuaji. Vifaa hivyo vimekabidhiwa hivi karibuni na Bohari ya Dawa (MSD). Mfamasia Kituo cha Afya Makorora Tanga Bi.Gloria Urio akionesha baadhi ya vifaa tiba kwaajili ya upasuaji walivyokabidhiwa na Bohari ya Dawa hivi karibuni baada ya kuwa na changamoto ya vifaa tiba hivyo na kutokutoa huduma ya upasuaji kwenye kituo hicho cha Afya Mkoani Tanga.Mfamasia Kituo cha Afya Ngamiani mkoani Tanga, Bw.Michael Mrosso akiangalia vifaa tiba ambavyo wamekabidhiwa na MSD hivi karibuni Jenerata ambalo litatumika kuzalisha umeme pindi umeme wa kawaida unapotokea kukatia katika Kituo cha Afya Ngamiani mkoani Tanga. Jenereta hilo limekabidhiwa na Bohari ya Dawa (MSD) hivi karibuni.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, TANGA
SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa imepongezwa kwa kuwezesha kukabidhi vifaa tiba katika vituo vya afya mkoani Tanga, vifaa ambavyo vilikuwa changamoto katika utoaji huduma kwa baadhi ya vituo vya afya kwenye mkoa huo.
Akizungumza leo Julai 17,2022 mara baada ya kutembelewa na watumishi wa MSD mkoani humo, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack amesema walipokea vifaa vya kufanyia upasuaji ikiwemo kitanda cha upasuaji, mashine ya dawa ya usingizi na taa zinazotumika wakati wa upasuaji ambavyo vimekuwa msaada mkubwa katika hospitali kwani mwanzo kulikuwa na changamoto kwnye hutoaji huduma.
"Awali tulikuwa hatufanyi upasuaji kabisa kwahiyo tulivyopokea fedha kwaajili ya ukarabati majengo kwaajili ya kufanyia upasuaji na tulifanya hivyo na baadae vifaa vililetwa na MSD na kuanza kutoa huduma za upasuaji". Amesema Dkt.Angelina
Amesema baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo walianza kutoa huduma ya upasuaji na kwasasa wanafanya upasuaji mbalimbali wa mama wajawazito pamoja na upasuaji mdogo kwani hapo awali walikuwa wanawapeleka wagonjwa Bombo kwasababu huduma hiyo haikuwepo hapo kituoni.
Aidha Dkt.Angelina amesema kwa siku wanapokea wamama takribani 60 lakini mwanzo walikuwa wanashindwa kutoa huduma na hata pale mama anakuwa na uzazi pingamizi usiku inakuwa ni changamoto kumkimbiza mama na kuchelewa kupata huduma kwa mama mjamzito.
"Kwa ujio wa vifaa hivi imerahisisha mama mjamzito anaposhindwa kujifungua moja kwa moja tunaweza kumpa huduma ya upasuaji na tunaokoa maisha ya mama pamoja na kachanga". Amesema.
Pamoja na hayo Dkt.Angelina amesema walikabidhiwa pia na jenereta kwaajili kuzalisha umeme kwenye hospitali hiyo lakini wakaamua kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu ili waweze kuichukua ili waikabidhi kwenye vituo vingine ambavyo haina jenerata kwasababu kituo hicho kilikuwa na jenerata ambalo walikuwa wameshanunua awali.
Ameeleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika kituo hicho ni nzuri kwasababu kunadawa ambazo zinahitajika kwa muda wote na ngazi ya kituo, dawa hizo wanazo kwa asilimia 90 na wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi .
Nae Mfamasia Kituo cha Afya Ngamiani mkoani humo, Bw.Michael Mrosso amesema walipokea vifaa tiba kwaaajili upasuaji pamoja na jenerata, vifaa ambavyo vilikuwa ni kilio kwao kwa muda mrefu.
Amesema wataendelea kujitahidi kutoa huduma bora kwakuwa kuna vifaa bora ambavyo wamekabidhiwa na serikali kwaajili ya kuwahudumia wananchi
0 comments:
Post a Comment