Homa kali, mwili kuchoka, shida ya kupumua na kutoka damu puani, ndizo dalili za awali ambazo zimeripotiwa za ugonjwa usiojulikana uliozuka huko Kusini mwa Tanzania.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichwale amebainisha dalili hizo alipozungumza na EAST Africa Radio.
"Timu bado ipo 'site', wakija {na ripoti kamili}, tutaeleza Umma sasa bado ni mapema.
"Mkoa wa Lindi wanajaribu kufuatilia hii shida ni nini?
"Dalili tulizoambiwa homa kali, mwili kuchoka, kupata shida ya kupumua na kutoka damu puani, ndizo wanazosema," amesema.
Dkt. Sichwale ameongeza"Timu yetu ya idara ya magonjwa ya dharura na majanga na nyingine kutoka Idara ya Kinga katika Kitengo cha epidemiolojia.
"Timu ya afya ya Mkoa na halmashauri na idara ya mifugo wanaendelea na ufuatilia, taarifa itatolewa na Waziri wa Afya, tuwe na subra" amesema.
Julai 13, 2022 {jana}, akizungumza katika Maadhimisho ya Mkutano wa 20 wa AMECEA, Rais Samia Suluhu Hassan alisema ugonjwa umeingia huko Kusini mwa Tanzania, watu wengi wanatoka damu puani na kudondoka.
"Ingekuwa mmoja tungesema labda ana 'presha' {Shinikizo la damu} au 'veins' zimepasuka {puani}, Lakini ni wengi wanadondoka kwa mara moja," alisema.
Ingawa hakubainisha takwimu, Rais Samia alithibitisha kwamba tayari wataalamu wa afya wamehamia {wamepiga kambi} huko wakifuatilia kwa kina ugonjwa huo.
Rais Samia ameongeza "Hatujui kitu gani wataalamu na wanasayansi wamehamia huko wanaangalia.
0 comments:
Post a Comment