Friday, 22 July 2022

HIZI HAPA DAWA UNAZOPASWA KUZIEUPUKA, ZINAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME

...
Tafiti mbalimbali zimegundua dawa ambazo zina athari kubwa juu ya nguvu za kiume na hutumiwa mara kwa mara.

Hapa chini ni dawa zinazopaswa kuepukwa na wanaume, ili wasipoteze nguvu zao za kiume.


Maisha ya kitandani ni moja ya mahitaji makubwa ya mwanadamu, lakini wakati mwingine huja na changamoto.


Sababu mbalimbali zinaweza kusababisha vikwazo hivi, lakini baadhi ya sababu zinahusishwa na aina sita ya dawa kama ilivyotangazwa na Shirika la Habari la ANI, ambalo lilitayarisha taarifa maalum juu ya mada hii.

Dawa ya kutuliza maumivu


Watu wengi hawasiti kutumia dawa za kutuliza maumivu hata kwa maumivu wanayohisi ni madogo.


Lakini, je, unajua kwamba dawa zilezile za kutuliza maumivu zinaathiri uanaume wako na kuufanya usiwe na matokeo mazuri kitandani?


Dawa za kutuliza maumivu huzuia kuundwa kwa seli za uzazi na huvuruga homoni nyingi ambazo ni muhimu katika kufanya tendo la ndoa kati ya wanaume na wanawake.

Dawa ya kuzuia wasiwasi (anti-anxiety)


Watu wengi wanaolalamika kuhusu matatizo ya akili na kuwa na wasiwasi hutumia dawa ili kukabiliana na hofu.


Walakini, dawa kama hizo hupunguza hamu ya tendo la ndoa.


Dawa hizi zinaweza kusababisha mtu kupoteza hamu ya kufanya mapenzi.


Wakati mwingine hata husababisha wanaume kupoteza fahamu zao kabisa.


Dawa ya kutibu kuganda kwa damu


Dawa zinazotumika kutibu kolesto, ambayo ni mgando wa damu, pia zina mchango mkubwa katika kupunguza nguvu za kiume.


Wataalamu wa matibabu wanasema kuwa dawa hizi huingilia utendaji wa seli za uzazi.


Utafiti unaonyesha kuwa dawa zinazotumika kutibu kuganda damu wakati mwingine husababisha matatizo kwa wanaume wanapolala kitandani na wake zao.


Dawa za msongo wa mawazo (Sonona)


Dawa hizi, zinazojulikana kama "benzodiazepines," mara nyingi hutumiwa kutibu magonjwa ya wasiwasi, kama vile wakati mtu anaogopa vitu ambavyo havipo na yuko peke yake.


Magonjwa mengine ambayo hutumia dawa hizi ni pamoja na kukosa usingizi na maumivu ya misuli.


Lakini, upande wa madhara ni kwamba huathiri utendaji wa seli za uzazi wa kiume na hisia.

Dawa ya Kuzuia Shinikizo la damu

Wagonjwa wanaotumia dawa za shinikizo la damu wanaweza pia kukumbana na changamoto nyingine ambayo ni kupungua kwa nguvu zao.


Dawa hizi zinaingiliana moja kwa moja na mishipa ya damu na pia hufanya kazi na mfumo wa neva.


Wataalamu wengine wameongeza kuwa yapo hata matatizo ambayo wanawake wenyewe wanakumbana nayo na dawa hizo ambazo zinahusiana na viungo vya uzazi.


Dawa za Kifua Kikuu


Dawa za dukani kama vile dawa za kupuliza katika pua zilizoziba na dawa za kwaida za kupunguza kuziba kwa pua zina athari zake.


zinaweza kusababisha matatizo katika tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.

Ongea na daktari


Zungumza na daktari wako ikiwa unafikiri kuwa dawa ina athari mbaya kwenye utendaji wako wa tendo la ndoa. Usiache kutumia dawa yoyote bila kwanza kuzungumza na mtoa huduma wako.

Chanzo - BBC Swahili


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger