Polisi huko Migori wanachunguza kisa ambacho kinaripotiwa kuwa mwanaume mwenye umri wa miaka 52 anadaiwa kuzimia na kufariki katika nyumba ya kulala wageni (Guest House) asubuhi ya jana ijumaa nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), marehemu; Naftali Nyandera, na mpenzi wake wa miaka 24 walikuwa kwenye nyakati nzuri kwenye nyumba ya kulala wageni kabla ya kifo chake.
"Katika kisa hicho ambacho kiliwashangaza wakazi wa Kanyarwanda, mwili wa Naftali Nyandera uligunduliwa ukiwa umetulia bila ya kutikisika kwenye kitanda katika nyumba ya kulala wageni ya Lavanda, baada ya shughuli nyingi zilizofanyika jioni na msichana huyo," ilisema taarifa ya DCI.
Uchunguzi wa awali wa DCI ulibaini kuwa mwanaume huyo alianguka saa chache baada ya kuingia chumbani na mwanamke huyo.
"Maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Macalder waliitwa katika eneo la tukio na kubaini kuwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 52 aliingia ndani ya chumba hicho akiwa ameongozana na msichana mwenye nusu ya umri wake, na kuzimia saa kadhaa baadaye kufuatia tukio la jioni," DCI alisema.
Mwili wa marehemu ulihamishwa kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Migori level IV ukisubiri uchunguzi wa maiti kufanyika.
0 comments:
Post a Comment