Wednesday, 27 July 2022

RADI YAUA WATU 22

...


NCHINI India imeripotiwa vifo vya watu 20 waliouawa na radi ikiwa ni ndani ya masaa 24 katika miji nane iliyo Mashariki mwa Jimbo la Bihar nchini humo.

Radi hizo ziliambatana na mwanga mkali ambapo Mkuu wa Jimbo la Bihar Nitish Kumar amewataka wananchi kufuatilia kwa ukaribu ushauri wa Mamlaka inayohusika na majanga nchini humo.


Mamia ya watu hufariki kila mwaka kutokana na radi ambazo mara nyingi hutokea kipindi cha mvua za Monsoon.

Sababu kubwa iliyotolewa ambayo inasababisha idadi kubwa ya vifo kwa raia wa India karibu kila mwaka kutokana na radi ni ule utamaduni wa watu wengi wa India kufanya kazi nje tofauti na mataifa mengine.

India imerekodi idadi ya radi milioni 18 kwa kipindi cha kuanzia Aprili 2020 hadi Machi 2021

Aidha siku ya jumanne Kumar alitangaza kiasi cha Rupee 40,000 ambayo ni sawa na Dola 5,008 kwa kila familia iliyofiwa.


Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba India imeripoti jumla ya radi milioni 18 katika kipindi cha Aprili 2020 hadi Machi 2021 na hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Climate Resilient Observing System Promotion Council ambalo pia limebainisha kuwa rekodi hizo ni ongezeko la 34% ukilinganisha na rekodi zilizopita katika kipindi kama hicho.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger