MASHEMASI Watano ambao wanatarajiwa kupewa daraja la Upadre hapo kesho, na askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, leo wamekiri imani Katoliki mbele ya askofu na Kanisa,ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utolewaji wa daraja la Upadre.
Mashemasi hao ambao ni Emmanuel Kimambo wa Parokia teule ya Shishiyu, Emmanuel Gembuya wa Parokia ya Buhangija, Paul Mahona wa Parokia ya Wila, Simon Lutamula wa Parokia ya Mwamapalala na Eliasi Vumba wa Shirika la Ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisco (Wakapuchini) wamekiri imani na kutia saini viapo vyao kupitia ibada ya masifu ya jioni, ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma,Ngokolo mjini Shinyanga.
Akitoa mafundisho yake katika ibada hiyo, Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu,anewaomba waamini kuendelea kuwaombea Mashemasi hao ili watakapopewa daraja la Upadre ,waweze kutekeleza kwa uaminifu utume watakaokabidhiwa na kanisa.
Askofu Sangu amefafanua kuwa, daraja la Upadre ambalo watapewa hapo kesho, ni njia itakayowashirikisha katika huduma ya kikuhani ya kuokoa roho za watu na kuwatafuta wale waliopotea.
0 comments:
Post a Comment