Sunday, 31 July 2022

UTEUZI: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA MARA

 


Share:

WAZIRI MKENDA AUNDA TUME KUCHUNGUZA UTOAJI MIKOPO KWA WANAFUNZI ELIMU YA JUU

Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda.


Na Mathias Canal, KILIMANJARO 

WAKATI dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2022/2023 likiwa wazi kwa muda wa siku 70 kuanzia Julai 19 hadi Septemba 30 mwaka huu, Serikali imetangaza Tume ya watu watatu kuchunguza utoaji wa mikopo.

Tume hiyo itaongozwa na Prof Allan Mushi ambaye ni mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Idd Makame kutoka Zanzibar na Dkt Martin Chegeni ambao wote kwa pamoja ni wataalamu wa mifumo waliyobobea katika sayansi ya Kompyuta na Takwimu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ametangaza tume hiyo tarehe 29 Julai 2022 Jijini Dar es laam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini juu ya mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema tume hiyo itachunguza uhalali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017/2018 mpaka 2021/2022 ili kubaini kama kulikuwa na upendeleo kwa watu wasiokuwa na sifa.

Waziri Mkenda amesema kuwa Tume hiyo pia itapitia malalamiko ya wanafunzi mbalimbali nchini ambao wamekuwa wakiyatoa kuhusu upendeleo wa utoaji mikopo kwa kupata mikopo kwa wanafunzi wenye sifa huku wale wasiokuwa na sifa stahiki wakikosa mikopo hiyo.
 
“Na kwenye hili tunakaribisha watu watoe taarifa kwa sababu kama kuna mtoto wa Mkenda uliyesoma nae utakuwa unamjua baba yake ni nani na uwezo wake, halafu wewe unaona mtu huyo amepewa mkopo toa taarifa” amesema Waziri Mkenda .

Pamoja na hayo ametahadharisha kuwa mtu yeyote ambaye ana wasiwasi na utoaji wa mikopo Wizara hiyo inamkaribisha ili aweze kuisaidia tume kufanya kazi yake kwa kuwa na taarifa zenye usahihi wa hali ya juu kutoka kwa wanachi husika.

Prof Mkenda amesema"Tume hii itaangalia vigezo vilivyoainishwa ili kuona kama kuna taarifa zingine za ziada zinaweza kutumika katika utoaji wa mikopo ili fedha zinazotolewa na serikali zikopeshwe kwa haki,"amesisitiza Mkenda.

Kadhalika, Waziri Mkenda amewahimiza waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2022/2023 kusoma na kuuzingatia ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa mwaka 2022/2023’ ili kuwasilisha maombi kwa usahihi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi zilizowekwa kwa mujibu wa taratibu na sheria.

Katika mwaka wa masomo 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha TZS 573 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo na Udhamini (Scholaship) kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini.


Share:

TANESCO DODOMA YAZIDI KUSHIKA KASI UTOAJI ELIMU KWA WANANCHI WANAONUFAIKA NA MIRADI WA REA.



Afisa Uhusiano na huduma kwa Wateja kutoka Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma Sarah Libogoma,akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnadani wakati akihamasisha pamoja na kutoa elimu kwa wananchi watakaonufaika na miradi ya REA jijini Dodoma.


Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Dodoma Bw.Madega Dudu,akitoa tahadharisha kwa wananchi dhidi ya utapeli na uhujumu miundombinu ya umeme Katika maeneo yao wakati wakiendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Mnadani watakaonufaika na miradi ya REA jijini Dodoma.

Diwani kata ya Mnadani Paul Bakinye ,akiishukuru TANESCO Mkoa wa Dodoma kwa kufika Katika kata yake kwa ajili ya kuhamasisha na kutoa elimu juu ya Miradi ya REA katika jiji la Dodoma.



Mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi huo Jijini Dodoma Marlon Bulugu,akielezea hatua za mradi zilipofikia wakati wa zoezi la kuhamasisha na kutoa elimu juu ya Miradi ya REA katika jiji la Dodoma.

WANANCHI wa Kata ya Mnadani wakiendelea kupata elimu juu ya Miradi ya REA katika jiji la Dodoma ikitolewa na Afisa Uhusiano na huduma kwa Wateja kutoka Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma Sarah Libogoma (hayupo pichani)

....................................



Na Alex Sonna-DODOMA



SHIRIKA la umeme nchini TANESCO Mkoa wa Dodoma linaendelea na uhamasishaji na utoaji Elimu maeneo yanayonufaika na miradi ya REA jijini Dodoma ambapo kufikia mwisho wa awamu hii ya miradi wananchi zaidi ya 30,000 wanatarajiwa kufikiwa na huduma.



Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnadani,Afisa Uhusiano na huduma kwa Wateja Mkoa wa Dodoma Sarah Libogoma , amesema kuwa miradi hiyo ya REA imelenga kujaziliza na kufikia maeneo yote ambayo umeme ulipita bila kusambazwa awamu zilizopita pamoja na kufikia maeneo ya pembezoni mwa Jiji.




"Kata ya Mnadani ni kata iliyonufaika na miradi miwili ya REA ile ya ujazilizi na ya pembezoni, ambayo umeme umeshawashwa na tunategemea kuunganisha wateja zaidi ya 350 kwenye kata hii". Amesema Libogoma



Ameongezea kuwa, pamoja na umeme kufika majumbani ni vyema wananchi walio eneo la mradi wakachangamka na kutumia fursa ya miradi hii kuweza kukuza uchumi binafsi na ule wa maeneo yao kwa kuomba huduma ya umeme mapema.



" Shirika limeboresha taratibu za uombaji huduma kwani sasa hakuna mambo ya fomu, kwa kutumia namba yako ya Nida utaomba umeme moja kwa moja TANESCO kupitia NiKONEKT ambapo kama una simu janja utapakua Nikonekt na kufanya maombi au kama ni kitochi utabonyeza *152*00# na kisha kufuata maelekezo ya kufanya ombi lako, hatuna mawakala wanaosajili maombi mtaani tafadhali tuepuke vishoka..."



Kwa upande wake Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Dodoma Bw.Madega Dudu,amewatahadharisha wananchi dhidi ya utapeli na uhujumu miundombinu ya umeme Katika maeneo yao kwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika utoaji wa taarifa za wazi na siri kwa TANESCO ili hatua zichukuliwe mapema.



"Mpaka umeme huu wa unafikishwa hapa umesafiri kutoka mbali sana na umepita katika njia salama ndio maana unawaka, hivyo ni jukumu mojawapo la sisi Wanambwanga na Wanandachi kiujumla kulinda miundo mbinu iliyopo hapa na kuhakikisha usalama muda wote kwani Shirika linaendelea na kubaini wahujumu na kuwachukulia hatua kama ambavyo sheria ya uhujumu inavyotaka", amesema Dudu



"Kumekuwa na wizi wa nyaya za umeme aina ya shaba ambazo zinafungwa kwenye mashine umba (Transformer) ambazo zimewekwa kwaajili ya ulinzi wa miundo mbinu ili kuepusha madhara lakini kumekuwa na watu ambao wamekosea uzalendo wanakata na kuiba zile nyaya na kuturudisha nyuma, kwaio ulinzi shirikishi ni muhimu kulinda hii miundo mbinu". amesema Dudu



Naye Mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi huo Jijini Dodoma Marlon Bulugu, amesema mradi kwa sasa upo ukingoni kazi inayoendelea ni kukamilisha uvutaji nyaya sehemu iliyobakia.



"Wiki lijalo tunakamilisha kazi ya uvutaji nyaya kwa nguzo zilizobakia, tunachohitaji ni muitikio wenu hivyo ni vyema wananchi mkaendelea na maombi ili nasi tuweze kukamilisha ufungaji mita mapema katika nyumba zenu".amesema Bulugu.



Naye Diwani kata ya Mnadani Paul Bakinye ameishukuru TANESCO kwa kufika Katika kata yake na kuelewesha wananchi wa mitaa yake juu ya miradi ya umeme na matarajio ya serikali kwenye kata yake kupitia miradi hii.


Uelimishaji huu unaendelea mtaa kwa mtaa mjini Dodoma katika kata zote zinazonufaika na miradi hii.



TANESCO Dodoma inasimamia utekelezaji wa miradi miwili ya REA inayoendelea ndani ya Jiji la Dodoma, miradi hii ni ya ujazilizi unaotekelezwa na mkandarasi Derm Electrics na ile ya pembezoni (peri-urban) unaotekelezwa na mkandarasi Cylex Engineering.


Mpaka sasa miradi hii imefikia 91% na 79% za utekelezaji wake ambapo tayari wateja zaidi ya 18,000 Mkoa mzima wamekwisha unganishiwa huduma.
Share:

SIMBA SC YAIBUKA NA SLOGAN MPYA "WE ARE UNSTOPPABLE".....HATUSHIKIKI HATUZUILIKI


CEO wa Simba Barbara Gonzalez Kushoto akizindua Slogan mpya kwa msimu huu We Are Unstoppable (Kushoto) ni malkia wa Bongo Fleva Zuchu
 **
Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema kuwa msimu huu klabu hiyo imejipanga kurudisha makombe yote ya ndani na kuhakikisha inafika nusu fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika.


Barbara ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa Simba Week uliofanyika Mbagala Zakheim Dar es salaam ambapo pia ameongeza kuwa usajili bado unaendelea na kuanzia wiki ijayo wataendelea kushusha wachezaji wengine.


“Safari hii hakuna kuteleza tena. Tumejipanga kuhakikisha tunarudisha mataji yote kuanzia Ligi Kuu, FA na kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika”


Kuelekea kilele cha Simba Day ambayo itafanyika Agosti 8, 2022 Simba imezindua Slogan Mpya We Are Unstoppable Hatushikiki Hatuzuiliki.

Msimu uliopita Simba ilizisiwa ujanja na watani zao Yanga baada ya kuzoa makombe yote ikiwemo la ligi kuu ya Nbc, pamoja na Kombe la shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup) na Ngao ya Jamii.
Share:

MKURUGENZI MKUU REA ASISITIZA UCHAPAKAZI KWA WATUMISHI


Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (Meza Kuu-aliyesimama), akizungumza na Wafanyakazi wa Wakala hiyo katika kikao maalumu kilichofanyika jijini Dodoma Julai 29, 2022.


Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (katikati), akizungumza na Wafanyakazi wa Wakala hiyo (hawapo pichani) katika kikao maalumu kilichofanyika jijini Dodoma Julai 29, 2022. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Adrophine Tutuba na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE, Tawi la REA, Swalehe Kibwana.


Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala, Mhandisi Hassan Saidy (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa REA katika kikao maalumu kilichofanyika jijini Dodoma Julai 29, 2022.


Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Tawi la REA, Swalehe kibwana akizungumza wakati wa kikao maalumu cha Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Saidy (katikati) na wafanyakazi wa Wakala hiyo kilichofanyika jijini Dodoma, Julai 29, 2022. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Adrophine Tutuba.

***************************

Na Veronica Simba - REA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amewataka wafanyakazi wote wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa weledi na kujituma ili kufikia malengo yake ya kuboresha maisha ya wananchi vijijini kwa kuwezesha upatikanaji wa nishati bora na zenye gharama nafuu.

Aliyasema hayo mwishoni mwa juma, Julai 29, 2022 wakati wa kikao maalum baina yake na wafanyakazi wa REA kilicholenga kujadili utendaji kazi, kusikiliza changamoto za watumishi na kuzitolea majibu.

Mhandisi Saidy aliwataka wafanyakazi wote kushirikiana na kuweka nguvu ya pamoja katika utekelezaji wa vipaumbele vya Wakala kwa sasa, ambavyo alivibainisha kuwa ni pamoja na kupeleka umeme vitongojini, programu ya kusaidia upatikanaji wa petroli vijijini, mradi wa kuwezesha upatikanaji wa nishati bora ya kupikia vijijini pamoja na kupeleka umeme katika visiwa.

Kuhusu usambazaji umeme vitongojini, alieleza kuwa ni mradi unaolenga kuvipelekea umeme vitongoji vyote ambavyo havijafikiwa na nishati hiyo, baada ya kila kijiji sasa kufikiwa na mradi wa umeme.

Alifafanua kuwa gharama ya mradi inakadiriwa kuwa shilingi trilioni 6.5 na kwamba katika mwaka huu wa fedha, shilingi bilioni 140 zimetengwa kwa ajili ya utambuzi wa wigo wa mradi pamoja na kuanza kazi ya utekelezaji wa mradi awamu kwa awamu.

Vilevile, aliuelezea mradi wa kuwezesha ujenzi wa vituo vidogo vya kusambaza bidhaa za petroli vijijini, ambapo alibainisha kuwa Serikali imeubuni ikilenga kuwezesha na kuendeleza vituo hivyo kwa maeneo ya vijijini ambayo hayana vituo vya mafuta kwa njia ya mkopo nafuu.

Alisema kuwa mradi huo ni wa majaribio ambao ni sehemu ya jitihada za kutafuta mbinu bora zaidi za kusambaza nishati ya mafuta salama na kwa bei nafuu vijijini.

Pia, Mkurugenzi Mkuu alifafanua kuwa katika mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga shilingi milioni 500 ili kufanya kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati bora ya kupikia pamoja na kuwezesha kufanyika kwa tafiti za kubaini nishati, mfumo sahihi na vivutio vya kusambaza nishati hiyo kwa maeneo ya vijijini.

Aliongeza kuwa, katika mwaka wa fedha 2022/23, shilingi bilioni 10 zitatumika kutekeleza mradi wa majaribio wa kupeleka na kusambaza gesi asilia katika makazi ya wananchi wanaopitiwa na mkuza wa bomba kuu la gesi katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani.

Aidha, kuhusu kipaumbele cha nne kinachohusisha upelekaji umeme visiwani na maeneo yaliyo mbali na Gridi ya Taifa, Mhandisi Saidy alieleza kuwa mradi unahusisha ujenzi wa miradi midogo midogo ili kuzalisha na kusambaza umeme kutokana na vyanzo vya nishati jadidifu kama vile jua, upepo, maporomoko madogo ya maji pamoja na tungamotaka.

Alitaja gharama ya mradi kuwa ni takribani shilingi bilioni 54 na kwamba katika mwaka huu wa fedha, shilingi bilioni 20 zimetengwa kutoka Serikali ya Tanzania.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu aliwahakikishia wafanyakazi wa REA kuwa changamoto mbalimbali zinazowakabili, zitaendelea kufanyiwa kazi ili kuzitatua na kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Tawi la REA, Swalehe Kibwana alimshukuru Mkurugenzi Mkuu kutenga muda wa kukutana na wafanyakazi ili kuzungumza nao na kupokea changamoto zao.
Share:

Video : BUGANGA - MAYEMU 'Bangi'

Hii hapa ngoma ya Msanii Buganga inaitwa Mayemu 'Bangi'
Share:

BANK OF AFRICA YAWAPATIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYABIASHARA MKOANI MWANZA


Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Adam Mihayo, akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara wateja wa benki hiyo iliyofanyika jijini Mwanza.
***

BANK OF AFRICA-TANZANIA imeendesha warsha ya uwezeshaji wajasiriamali iliyolenga wafanya biashara wadogo na wakati (SME) mkoa wa Mwanza. Tukio hili liliwakutanisha pamoja wateja mbalimbali wa benki hiyo ambao ni Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (SME) na kuwapatia ujuzi na maarifa muhimu kwa ukuaji mzuri na thabiti ya biashara zao.

Washiriki kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mwanza, walijengewa uwezo kuhusu masuala ya kifedha ikiwemo mbinu za utunzaji fedha, namna ya kukuza mtaji na kushirikiana ili kukua pamoja kibiashara.

Akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA, Bw. Adam Mihayo, aliwahimiza wajasiriamali na wafanyabiashara nchini kuchangamkia huduma za kifedha zitolewazo na Benki hiyo ili kuongeza tija.

"Sisi BANK OF AFRICA, katika mpango mkakati wa miaka mitatu ni kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Sekta ya wafanyabiashara wadogo na wakati ni sekta muhimu na nyeti katika uchumi wetu inachangia asilimia 30% katika pato la taifa. Ukiangalia takwimu katika biashara 10, 9 zitatokea kwa wafanya biashara wadogo na wakati. 

Nawakaribisha Bank of Africa kwa kuwa ndiyo benki yenye mtazamo chanya unaolenga kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wakati, hii ni katika huduma zetu madhubuti kwenye sekta hii kuanzia ufunguaji wa akaunti ya benki, mikopo, ufumbuzi wa kibiashara na ushauri katika kukuza na kustawisha biashara za wajasiriamali. Karibuni tuwahudumie” alisema, Bw Adam Mihayo.


Bw. Adam Mihayo, pia alisema kwa kipindi cha mwaka jana Benki ilitoa mikopo ya kiasi cha shilingi bilioni 32 kwa wajasiriamali wadogo na wakati, ukilinganisha na mwaka huu mpaka juni mwaka huu tayari imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 23 huu ni mwenendo mzuri na tunatumaini kwamba mpaka mwisho wa mwaka tutakua tumetoa kiasi kikubwa zaidi.

“Katika mpango mkakati wa miaka mitatu pia tumepanga kutoa mikopo ya kiasi cha shilingi bilioni 132 kwa sekta hii nyeti na tunaamini katika kufanya hivyo tunachangia ukuaji wa uchumu wetu. 

Dhumuni kubwa la warsha hii ni kuwawezesha wafanyabiashara wa jijini Mwanza ambao ni wateja wetu katika maeneo mbali mbali, utafiti unaonyesha kwamba biashara nyingi hazifanikiwi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati ni kutotunza kumbukumbu vizuri, wanapata changamoto ya mahesabu yao, kunachangamoto pia ya dhamana. Mada za warsha hii zitawawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi.

Tunaamini kwamba sisi kama BANK OF AFRICA, tunaendelea vizuri kibiashara. Ukiangalia mahesabu yetu tumeweza kukuza mizania yetu (balance sheet) mpaka kufikia shilingi bilioni 711, ukuaji ambao hatujawahi kufikia, faida yetu pia imekua kwa asilimia 37 ukilinganisha juni mwaka jana faida ya shilingi bilioni 3.4 na Juni mwaka huu ya shilingi bilioni 4.7. Tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kufikia mahitaji ya wateja wetu” alisemaBw. Mihayo.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria warsha hiyo, wameipongeza BANK OF AFRICA, kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa BOA, Bi. Ninael Mndeme, amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati wote katika benki hiyo kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.
Baadhi wa Wajasiriamali waliohudhuria warsha ya kuwajengea uwezo kibiashara iliyoandaliwa na BOA wakifuatilia mada mbalimbali.
Baadhi wa Wajasiriamali waliohudhuria warsha ya kuwajengea uwezo kibiashara iliyoandaliwa na BOA wakifuatilia mada mbalimbali.
Baadhi wa Wajasiriamali waliohudhuria warsha ya kuwajengea uwezo kibiashara iliyoandaliwa na BOA wakifuatilia mada mbalimbali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa River Oil Gabriel Kenene (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa benki ya BOA wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Adam Mihayo (wa pili kutoka kulia) wakati walipomtembelea ofisini kwake.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Khalii(kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank Of Africa (BOA), Adam Mihayo alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji Wa BOA,Adam Mihayo akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza
Share:

MGAWO WA UMEME KATIKA VIJIJI 20 LUDEWA WAPATIWA UFUMBUZI NA MAKAMBA


Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akizungumza na Wananchi katika Kijiji cha Lugarawa wilayani Ludewa baada ya kufika kijijini hapo kutatua changamoto ya upatikanaji umeme.

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akimsikiliza mmoja wa Wananchi katika Kijiji cha Lugarawa wilayani Ludewa baada ya kufika kijijini hapo kutatua changamoto ya upatikanaji umeme.


Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akizungumza na mmoja wa Wananchi katika Kijiji cha Lugarawa wilayani Ludewa baada ya kufika kijijini hapo kutatua changamoto ya upatikanaji umeme.

**************************

Waziri wa Nishati, Mhe Januari ametoa ufumbuzi wa changamoto ya miaka mingi ya mgawo wa umeme wa masaa 12 kwa vijiji 20 katika Wilaya ya Ludewa ambavyo vimekuwa vikipata umeme kutoka kampuni ya Madope.

Kampuni hiyo ya Madope inayoendesha mradi huo mdogo wa umeme wa maji (MW 1.7 inaundwa na wadau mbalimbali wakiwemo Jumuiya ya Watumia Umeme Lugarawa na Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.

Changamoto hiyo ya mgawo wa umeme imetokana na waya unaotumika kusambaza umeme kuwa mdogo ukilinganisha na mahitaji ya wananchi ambao wanaotumia umeme kwa shughuli za kiuchumi kama vile kuendesha mashine za kukamulia alizeti na kukoboa na kusaga nafaka.

Akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Lugarawa wilayani humo, Waziri Makamba amesema kuwa, Serikali kupitia TANESCO imeamua kununua umeme wote unaozalishwa na kampuni hiyo baada ya kufanya mazungumzo na wadau wote wanaohusika na mradi huo pamoja na TANESCO.

Amesema kuwa, kwa TANESCO kununua umeme huo kutawezesha wananchi kupata umeme wa uhakika kwani kwa sasa katika megawati 1.7 zinazozalishwa, umeme unaotumika ni 0.3 na pia kampuni hiyo ya Madope itapata mapato.

Ameongeza kuwa, Wataalam wa TANESCO watafika Lugarawa tarehe 7 Agosti 2022 ili kufanya tathmini ya Miundombinu ya Usafirishaji umeme pamoja na kusaini mikataba ya makubaliano hayo na inategemewa kuwa ifikapo mwezi wa Pili mwaka 2023 wananchi hao watakuwa wameshaanza kupata umeme wa uhakika.

Mradi huo wenye wateja 3200 kwa sasa umeleta manufaa mbalimbali kwa wananchi wa Kijiji hicho ikiwemo kutoa huduma ya umeme katika vituo vya afya, shule za Sekondari 5, shule za msingi 19 na kituo kimoja cha kulelea watoto yatima.

Utekelezaji wa Mradi wa umeme wa Madope umewezeshwa na wadau mbalimbali ikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao ulitoa shilingi Bilioni 4.5 kuendeleza mradi huo.

Wananchi pamoja na viongozi katika Wilaya hiyo akiwemo Mbunge wa Ludewa,, Mhe. Joseph Kamonga wamemshukuru Waziri wa Nishati kwa kutoa ufumbuzi wa changamoto hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu.

Akiwa wilayani humo Waziri wa Nishati ameendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia ambapo ametoa mitungi ya gesi kwa kinamama ikiwa ni mradi wa majaribio utakaofanyiwa tathmini ili Serikali itengeneze mkakati bora wa kitaifa wa namna bora ya kusambaza nishati hiyo nchini.

Share:

Saturday, 30 July 2022

SERIKALI INAPAMBANA KUTATUA CHANGAMOTO YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU


********************

Naibu Waziri Mary Masanja (Mb) amesema kuwa Serikali itahakikisha inapata ufumbuzi wa changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu wanaovamia Makazi ya watu hususan tembo.

Ameyasema hayo leo katika ziara ya kikazi alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) mjini Morogoro. Amesema kuwa Serikali haifurahishwi na matukio ya wananchi kuuawa na tembo au kuliwa mazao yao.

"Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan haifurahii matukio ya tembo kuuwa watu kwa sababu uhai wa mtu hauwezi kurudishwa" Mhe. Masanja amesisitiza

Amesema moja ya mikakati ya kutatua changamoto hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na tembo.

Ameongeza kuwa njia nyingine ya kutatua tatizo hilo ni kuwavisha tembo viongozi kola maalum ili kuwawezesha Askari Uhifadhi kujua mwelekeo wa kundi la tembo.

Pia, amesema Serikali inaendelea kutafuta mbinu za muda mrefu za kutatua changamoto hiyo.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za kusikiliza changamoto za Taasisi na kuangalia utekelezaji wa majukumu yake iili kutafuta ufumbuzi.
Share:

DON BOSCO DIDIA YATANGAZA NAFASI ZA KUJIUNGA NA FORM ONE 2023

 

Share:

MWANAMKE AISHI NA MAITI YA KAKA YAKE...MWENYEWE ADAI NI MUNGU

Polisi mjini Kakamega nchini Kenya wamemzuilia mwanamke wa makamo kwa madai ya kuishi na maiti kinyume na sheria.

Shamim Kabere, mkazi wa Iyala, eneo bunge la Lurambi, anasemekana kuuhifadhi mwili wa Ainea Tavava, 48, ndani ya nyumba yake kwa zaidi ya siku 10.

Juhudi za wakazi kutafuta chanzo cha uvundo huo usiokuwa wa kawaida ziliwafikisha hadi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo ambapo walilazimika kuvunja mlango wake na kukuta mwili wa mtu ukioza kitandani.

"Nzi na ndege wengi walikuwa wakizunguka nyumba ya mshukiwa iliyokuwa inanuka, jaribio letu la mara moja kubaini chanzo cha harufu hiyo lilikuwa hadi wakati nzi walianza kujaa nyumbani kwake.

"Mwili uliooza ukitoka funza ulikuwa umelala kitandani, ishara kwamba aliaga dunia muda mrefu uliopita," alisema Josephine Nawire, jirani wa mshukiwa. 

Kulingana na wakazi wa eneo hilo, aliyejiita mungu huyo na mtumishi wake walihamia kijijini humo miezi michache iliyopita.

 Waliishi maisha ya siri, hawakuwahi kutangamana na wengine.


Shamim alikiri kuishi na maiti hiyo akisema ni mungu wake na aliamriwa kufungiwa ndani ya chumba hicho kwa siku nyingi ili kuombea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9. 

"Kati ya siku 14 zilizohitajika, 9 zilikiwa tayari zimekamilika. Hapo awali alikuwa amenionya dhidi ya kufungua mlango kabla ya siku zilizotajwa kuisha," alisema.

 Chifu wa eneo hilo Simon Aketch alithibitisha kisa hicho akiwaomba wakaazi kuwa watulivu huku uchunguzi kuhusu suala hilo ukianzishwa.

“Mshukiwa alitumia chumba kimoja huku mwili wa mwathiriwa ukiwa katika chumba kingine, alidai kuwa hakufahamu ulikotoka uvundo huo. 
Polisi kutoka kituo cha Kakamega wameanza uchunguzi,” alisema.

 Kwa mujibu wa sheria za Kenya, mara baada ya mtu kufariki dunia akiwa nyumbani, wale walio karibu na mwili huo wanapaswa kupiga ripoti kwa chifu, ambao huwasiliana na idara ya afya na kuanza taratibu za kisheria za kushughulikia mwili huo.

Chanzo - Tuko News
Share:

AKUTWA AMEFARIKI GESTI BAADA YA KURUSHANA ROHO NA MREMBO


Polisi huko Migori wanachunguza kisa ambacho kinaripotiwa kuwa mwanaume mwenye umri wa miaka 52 anadaiwa kuzimia na kufariki katika nyumba ya kulala wageni (Guest House) asubuhi ya jana ijumaa nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), marehemu; Naftali Nyandera, na mpenzi wake wa miaka 24 walikuwa kwenye nyakati nzuri kwenye nyumba ya kulala wageni kabla ya kifo chake.

"Katika kisa hicho ambacho kiliwashangaza wakazi wa Kanyarwanda, mwili wa Naftali Nyandera uligunduliwa ukiwa umetulia bila ya kutikisika kwenye kitanda katika nyumba ya kulala wageni ya Lavanda, baada ya shughuli nyingi zilizofanyika jioni na msichana huyo," ilisema taarifa ya DCI.

Uchunguzi wa awali wa DCI ulibaini kuwa mwanaume huyo alianguka saa chache baada ya kuingia chumbani na mwanamke huyo.

"Maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Macalder waliitwa katika eneo la tukio na kubaini kuwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 52 aliingia ndani ya chumba hicho akiwa ameongozana na msichana mwenye nusu ya umri wake, na kuzimia saa kadhaa baadaye kufuatia tukio la jioni," DCI alisema.

Mwili wa marehemu ulihamishwa kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Migori level IV ukisubiri uchunguzi wa maiti kufanyika.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 30,2022





Magazetini leo Jumamosi July 30 2022














Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger