Wednesday, 12 May 2021

UBALOZI WA PALESTINA NCHINI TANZANIA UNAANGAZIA UHALIFU WA ISRAELI DHIDI YA WATU WA PALESTINA

...

 
Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania unaangazia uhalifu wa Israeli dhidi ya watu wa Palestina katika Yerusalem ya Mashariki iliyoko chini ya ukoloni na ukalizi wa Israeli.

Yerusalemu ya Mashariki ni sehemu muhimu ya nchi ya Palestina. Tangu kukaliwa kwake na ardhi kuporwa kutoka kwa Wapalestina kinyume na sheria za kimataifa mnamo mwaka 1967, Israeli imeweka lengo na utaratibu wa kubadilisha hali ya kisheria ya jiji, kudhibiti na kubadilisha muundo wa idadi ya watu waishio hapo.

Kupitia sera za kibaguzi na kwa kukiuka sheria Za Kimataifa kama ilivyoelezewa na ripoti ya Haki za Binadamu, iliyotoka hivi karibuni; Israeli ina nia ya kuunda kwa makusudi, ukweli mpya juu ya ardhi ya Wapalestina. Kuwezesha hilo, Israel imekuwa ikihamisha maelfu ya mamia ya watu wa Palestina kwa nguvu na kuwaondosha katika makazi yao ya miaka mirefu na kisha kuikabidhi kwa walowezi wa Israeli. Zaidi ya walowezi 200,000 wanaishi katika makazi haramu mjini humo, Mashariki ya Yerusalem. Israel yaendelea na upanuzi wa makazi haya katika ardhi ya Wapalestina kama ilivo sasa katika mtaa wa Sheikh Jerrah huko mjini Yerusalemu ya Mashariki ampapo famia saba za Wapalestina zalazimishwa kuondoka katika makazi yao.

HalikadhalikaIsraeli katika harakati zake kuufanya mji wa Yerusalemu kuwa mji wa Kiyahudi hufanya mashambulio yake ya kimfumo dhidi ya waumini wa Palestina wa dini za Kikristo na Kiislamu. Jeshi la Israeli limekuwa likivamia na kushambulia waamini wa Kikristo na Kiislamu hasa katika sherehe zao za dini mjini Yerusalemu mashariki. Wanajeshi wa Israeli mara kwa mara huzuia waumini wa Kiislamu wa Palestina kuingia ndani ya msikiti wa Al – Aqsa kwa ajili ya sala

Kulingana na ripoti ya Human Rights Watch ambayo ilichapishwa mnamo mwezi Aprili mwaka huu, Israeli inaendelea kuonyesha ukandamizaji na vitendo visivyo vya kibinadamu dhidi ya watu wa Palestina kwa nia ya kudumisha utawala wa kikabila unaowapa ukuu Wayahudi juu ya Wapalestina.

Ripoti hiyo ilihitimisha kwa kusema kuwa, Israeli inatekeleza utawala katili wa ubaguzi wa rangi ambao umesababisha miaka 54 ya ukoloni na makazi haramu katika ardhi ya Palestina na hivyobasi kukiuka sheria na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania unaangazia msimamo wa serikali ya Palestina kuhusu unyama huu unaofanywa na Israeli dhidi ya Wapalestina.

Akiongea na waandishi wa habari hivi leo, Balozi wa Palestina nchini Mh. Hamdi Mansour AbuAli ameitaka jumuiya ya kimataifa kutokaa kimya mbele ya uhasama na ukatili huu unaotendeka dhidi ya Wapalestina katika ardhi yao. Balozi amesema kuwa huu ni wakati muafaka kwa hatua ya kimataifa kutumia njia na hatua zinazoelezwa na sheria za kimataifa na hatimaye kuifanya Israeli na mashirika ya walowezi kuwajibika kwa ukiukaji wao na uhalifu dhidi ya watu wa Palestina.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger