Rubani wa zamani wa shirika moja la ndege la Marekani amekiri kufanya " kitendo kisichofaa" akiwa safarini mwaka jana.
Michael Haak, 60, alitoa nguo mbele ya rubani mwenzake wa kike ndani ya chumba cha marubani huku akitazama filamu za ngono (ponografia) kwenye kompyuta yake ndogo, waendesha mashtaka walisema.
Wakati ndege ya shirika la Southwest Airlines ikiendelea na safari, Haak aliendelea kufanya" kitendo kisichokuwa na staha " katika chumba cha marubani.
Jaji wa mahakama ya Maryland amemhukumu kifungo cha mwaka mmoja na kumuamuru alipe faini ya dola 5,000 sawa na (Pauni 3,500).
Tukio hilo lilitokea wakati ndege ilipokuwa safiri kutoka Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Philadelphia kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orlando mnamo Agosti 10 mwaka 2020, mahakama ilifahamishwa.
Wakati ndege iliposhika mkondo wa safari, Haak aliondoka katika kiti cha rubani, "kimakusudi" na kuanza kutazama filamu ya ngono kwenye kompyuta yake ndogo.
"Haak aliendelea kufanya tabia mbaya, huku rubani mwenzake wa kike akiendelea na kazi," taarifa ya waendesha mashtaka ilisema.
Haak hakuwahi kukutana na rubani mwenzake kabla ya safari hiyo, waliongeza.
Wakili msaidizi Michael Cunningham alisema rubani mwenzake "alikuwa na haki ya kutofanyiwa kitendo kama hicho, bila kujali ni nini kingechochea au kilisababisha kitendo hicho", Associated Press iliripoti.
Haak alishtakiwa Maryland kwasababu ndege ilikuwa ikipaa katika anga za jimbo hilo wakati wa tukio hilo. Alikiri kufanya hatia hiyo kimakusudi, hadharani.
Katika taarifa iliyowasilishwa kupitia link ya video, Haak aliomba msamaha kwa kufanya kitendo hicho, akisema: "Ilianza kama utani kati yangu na rubani mwenzangu. Sikudhani ingeligeuka kuwa hivi ndani ya miaka elfu moja."
Jaji wa mahakama ya Marekani, J Mark Coulson alimwambia Haak kwamba tabia yake ilikuwa na athari mbaya kwa rubani mwenzake na ingeweza kuathiri usalama wa abiria.
Haak, kutoka Longwood, Florida, alikuwa rubani wa shirika la Southwest Airlines kwa miaka 27 kabla ya kustaafu mwisho wa mwezi Agosti mwaka jana.
Katika taarifa, shirika hilo lilisema haliruhusu "tabia kama hiyo na itachukua hatua mara moja endapo mwenendo kama huo utathibitishwa". Msemaji alisema kampuni hiyo ilifahamishwa kuhusu tukio hilo baada ya Haak kuacha kazi kwa hiari.
Kampuni hiyo ilisema, imesitisha kumlipa mafao yoyote ambayo alikuwa anastahili kupata kama haki ya kustaafu.
CHANZO - BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment