Monday 31 May 2021

SHINDANO LA MISS KAHAMA KUFANYIKA JUMAMOSI HII JUNI 5

...
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (wa tano kulia)  akiwa na mwaandaaji wa Mashindano ya Miss Kahama, Peter  Frank Alex pamoja na baadhi ya washiriki wa shindano la Miss Kahama 2021
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shindano la Urembo kutafuta mlimbwende wa Kahama ‘Miss Kahama 2021’ yanatarajia kufanyika Jumamosi hii June 5,2021 katika ukumbi wa African Lounge Mjini Kahama yakishirikisha warembo 12 huku Msanii Mr. Blue akinogesha mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners ambao ni waandaaji wa Shindano la Urembo la Miss Kahama, Peter Frank Alex amesema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika.

Amesema shindano la Miss Kahama litafanyika Jumamosi hii June 5, 2021 African Lounge. Washiriki wapo 12 ambao ni mabinti warembo kutoka Kahama ambao sasa wapo kambini wanaendelea na mazoezi.

“Maandalizi ya shindano la Miss Kahama ni makubwa hivyo wananchi wategemee mambo makubwa siku hiyo kuanzia saa moja usiku. Tiketi zinaendelea kutolewa maeneo mbalimbali ikiwemo Huheso FM kwa Zakazi, BSL College, African Lounge na tunasambaza mtaa kwa mtaa na siku ya shindano tiketi zitapatikana getini”,amesema.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger