Friday 28 May 2021

WAZIRI UMMY AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WANNE UBADHIRIFU UJENZI MACHINJIO MANISPAA YA SHINYANGA

...

 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu akiwa kwenye ujenzi wa mradi wa machinjio ya kisasa Shinyanga.

Na Mwandishi wa  Malunde 1 blog

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi wiki mbili watumishi Wanne wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupisha uchunguzi tuhuma ubadhirifu ujenzi wa machinjio ya mifugo ya kisasa.


Watumishi walio simamishwa kazi ni Mchumi Gwakisa Mwakyeba, Mkuu wa idara ya Mifugo Tito Kagize, Mhandisi wa ujenzi Kasimu Thadei, pamoja na Mkuu wa idara ya manunuzi Godfrey Mwangairo.


Waziri Ummy akizungumza jana kwenye ujenzi wa mradi wa machinjio hiyo ya mifugo ya kisasa, mara baada ya kupewa taarifa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi na kuonekana kuna ubadhilifu wa fedha, ndipo akaamua kuwa simamishwa kazi watumishi hao ili kupisha uchunguzi.


Alisema Taarifa za mradi huo anazo kutoka kwa Mkukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuwa kuna ubadhirifu wa fedha kwenye machinjio hiyo, hivyo anashaghaa watu ambao waliohusika kutochukuliwa hatua.


"Mkurugenzi wewe ni mteule wa Rais hivyo sitakugusa kwenye suala hili, saizi yangu ni hawa watumishi, hivyo kuanzia sasa na wasimamisha kazi wiki mbili ili kupisha uchunguzi juu ya ubadhirifu wa ujenzi wa machinjio hii ya kisasa," alisema Mwalimu.


"Kuna watumishi wengine najua wameshahamishwa hapa Shinyanga, hivyo naagiza waletwe hapa ili kujibu  ubadhirifu wa ujenzi wa machinjio hii ya mifugo ya kisasa, pamoja na Wakandarasi wachukuliwe hatua,"aliongeza.


Aidha alisema gharama za ujenzi wa machinjio hiyo anazifahamu ni Sh. bilioni 5.7 na zimeshatumika bilioni 5.1 na kuhoji juu ya Sh. milioni 600 mahari zilipo, huku mradi huo ukiwa bado haujakamilika na kutakiwa tena kuongezwa Sh. 172 kutoka kwenye mapato ya ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Godfrey Mwangulumbi, akitoa taarifa ya ujenzi wa machinjio hiyo, alisema gharama za mradi huo awali ilikuwa ni Sh. bilioni 5.9, lakini zikapungua hadi Sh. bilioni 5.5 na zimeshatumika Bilio 5.1 huku akibainisha fedha Milioni 600 zipo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati, alisema suala la watumishi hao atalifanyia kazi na watatoa taarifa ndani ya wiki mbili ambazo zimetolewa.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger