Saturday, 29 May 2021

WAJASIRIAMALI WAASWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE BORA

...

 

**********************

Wajasiriamali kote nchini wameaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na kimataifa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya SIDO kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Kwaraa Babati mkoani Manyara.

Naye Meneja wa Uthibiti Ubora wa TBS Bw.Gervas Mwanjabala akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo, alisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya TBS kutoa elimu ya masuala ya viwango kwa wajasiriamali waliokusanyika kutoka sehemu mbalimbali nchini na vilevile n fursa ya kusikiliza maoni na changamoto za wajasiriamali na wananchi kwa ujumla na kutafutia ufumbuzi changamoto hizo.

.“Ushiriki katika haya maonesho umetufanya tuweze kukutana na wadau wenye viwanda,wananchi, wajasiriamali na kuweza kuwaelimisha kuhusu masuala ya viwango pamoja na kusikiliza changamoto zao”. Amesema Bw. Mwanjabala.

Aidha Meneja wa kanda ya kaskazini wa TBS, Bi. Happy Brown aliwataka wajasiriamali wote katika kanda hiyo kutosita kutoa taarifa zozote ili waweze kusaidiwa na hata kupatiwa ushauri wa kitaalam ili waweze kuzalisha bidhaaa bora.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa TBS Bi. Deborah Haule amesema muitikio wa watu katika maonesho haya umekuwa mkubwa na wajasiriamali wengi wamejitokeza kutaka kufahamu zaidi kuhusiana na taratibu za kufuata ili kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.

Amesema wajasiriamali wadogo nchini hawaingii gharama zozote bali wanatakiwa kupitia SIDO ili watambulike na wakipata alama ya ubora wanaweza kufikia masoko mbalimbali hasa ya Afrika Mashariki na zitaweza kuvuka mipaka ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote.

Pamoja na hayo Bi. Deborah amesema TBS inawahimiza wahakikishe wanazalisha bidhaa zilizo na ubora hatua itakayosaidia kulinda mitaji yao na kuhimili ushindani kwenye soko la kitaifa na kimataifa.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger