Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetangaza kusitisha safari zake kwenda nchini India ambako vifo na maambukizo ya corona yanazidi kuongezeka.
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji na ofisa mtendaji mkuu wa shirika hilo, Ladislaus Matindi inasema safari hizo zimesitishwa kuanzia Mei 4.
“ATCL itaondoa faini zote kutokana namabadiliko haya, itatoa tiketi nyingine au kuwarudishia nauli zao abiria waliokuwa wamekata tiketi,” amesema Matindi.
Ili kupata ufafanuzi zaidi, Matindi amewataka abiria waliokata tiketi kupiga namba O800110045 bure.
0 comments:
Post a Comment