Wednesday, 5 May 2021

RAIS SAMIA : MNA BAHATI KWAMBA UPANDE MMOJA KUNA UHURU NA UPANDE MWINGINE KUNA SULUHU

...

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema nchi yake iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya nchini mwake. Samia ambaye amewahutubia wafanyabiashara kutoka Kenya na Tanzania amesema hakuna nchi inayoweza kunawiri pekee yake bila ushirikiano.

Rais Samia amewatia shime washiriki katika mkutano huo kwa kusema kwamba wawekezaji hawafai kushindwa kuwekeza katika mataifa hayo mawili aliposema;

"Mna bahati kwamba nchi zetu mbili upande mmoja kuna Uhuru wa kufanya biashara na upande mwingine kuna Suluhu ya kuondosha vikwazo vya biashara.

Rais Samia amesema serikali yake imechukua hatua ya kuleta mageuzi ili kufanya mazingira ya kufanya biashara kuwavutia wawekezaji kutoka Kenya kwa lengo la kutumia fursa zilizopo .

Amesema Tanzania ina ardhi, vivutio vya utalii na raslimali ambazo zinaweza kutumiwa kuboresha hali ya kiuchumi wa mataifa yote mawili. 

Ameongeza kwamba sekta binafisi ni nguzo muhimu sana ya kuhakikisha kwamba nafasi za ajira zipo kwa wananchi wa mataifa yote .


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger