Rudisheni pesa zetu, ndizo kauli za mashabiki baada ya kutangazwa kuahirishwa kwa mchezo wa Simba dhidi ya Yanga leo Mei 8, 2021.
Mchezo wa Simba dhidi ya Yanga ulipangwa kupigwa leo saa 11:00 jioni na baadae kusogezwa mpaka saa 1:00 usiku kitendo ambacho Yanga walikigomea.
Uongozi wa Yanga umesema umepokea kwa masikitiko taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuhusiana na kusogezwa kwa mechi kutoka saa 11:00 hadi 1:00 jioni.
Wamesema Mabadiliko hayo ni kinyume cha kanuni ya 15(10) za Ligi Kuu inayohusu taratibu za michezo ambayo unasema mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote mbili husika za mchezo angalau masaa 24 kabla ya muda wa awali.
Uongozi wa Yanga umeitaka bodi ya Ligi na TFF kuendesha ligi kwa kuheshimu na kufuata kanuni zinazowekwa.
Basi la timu la Yanga limefika uwanjani saa 10:18, wakati Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mshindo Msolla amefika saa 10:05.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mchana huu imesema kwamba wamepokea agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuisogeza mbele mechi hiyo hadi Saa 1:00 usiku.
Dakika 15 pekee ziliwatosha Yanga kusubiri kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Simba na baada ya kuona hakuna timu wala waamuzi wanaoingia uwanjani hapo waliondoka na kurudi katika vyumba vya kubadilishia nguo.
Wakati wanaondoka majukwaa yaliyokuwa ma mashabiki wa timu hiyo yaliinuka kwa shangwe na kuishangilia timu yao huku wengine wakiondoka uwanjani hapo.
Ilipofika saa 11:35 wachezaji wa Yanga walitoka vyumbani na kupanda gari lao na kisha waliondoka uwanjani.
Wakati gari likitoka uwanjani mashabiki walikuwa wakiswasindikiza huku wakiimba “TFF, TFF ”, na kulifuata gari kwa nyuma.
Baada ya Yanga kuondoka uwanjani hapo, mashabiki wa Simba walionekana kupoa huku wale wa Yanga wakiendelea kushangilia na kuondoka uwanjani hapo mdogo mdogo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilisema mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni sasa itaanza saa 1 usiku.
TFF ilisema imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
TFF ilisema imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mchezo huo marudiano wa msimu baada ya miamba hiyo kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Novemba 7, mwaka jana utaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya AzamSports1HD ya Azam TV.
Mechi ya kwanza hapo hapo Benjamin Mkapa, Yanga SC walitangulia kwa bao la penalti la mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong kipindi cha kwanza, kabla ya beki Mkenya, Joash Onyango kuisawazishia Simba mwishoni kipindi cha pili.
0 comments:
Post a Comment