Na Andrew Chatwanga,Songea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma Simon Maigwa amewaambia waandishi wa habari leo kuwa tukio hilo limetokea Mei 19 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi.
Alisema kuwa Nombo alikuwa na wivu wa kimapenzi kwa mke wa Nchimbi na kuamua kumuua kwa kumchoma na kisu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda Maigwa alisema kuwa Bw. Nombo alinogewa na mapenzi ya mke wa marehemu Nchimbi kiasi cha kupelekea kuvunja ndoa yao na wivu uliomfanya afanye maamuzi ya kumuuwa mwenye mke ili apate nafasi ya kuwa huru na mke wa Bw. Nchimbi.
Aidha Kamanda Maigwa ametoa wito kwa watu wenye uhasama kupeleka matatizo yao katika vyombo vya usuluhishi badala ya kujichukulia maamuzi ambayo yanagharimu maisha ya watu na kuishia jela.
Wakati huo huo Kamanda Maigwa ameelezea uchunguzi wa tukio la mwananfunzi aliyejinyonga kwa kutumia kamba ya manila Sophia Mbano (19)mwananfunzi wa kidato cha tano katika sekondari wa wasichana ya St. Agnes Peramiho chanzo kimebainika kuwa ni msongo wa Mawazo ambao umepelekea kifo chake.
0 comments:
Post a Comment