Wednesday, 5 May 2021

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MIKUBWA YA MAJI JIJINI DODOMA

...

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kilimo,Mifugo na Maji Christina Ishengoma.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imetembelea  miradi mikubwa ya maji ya Mzakwe na Buigiri iliyopo jijini Dodoma  huku ikiridhishwa na mwendelezo wa utekelezaji wa  miradi hiyo.

Akizungumza  katika ziara hiyo Mei 4,2021 ,Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kilimo,Mifugo na Maji Christina Ishengoma ameipongeza  Wizara ya Maji kwa kuendelea kutekeleza miradi hiyo kwa ufasaha.

“Baada ya kuzunguka na kuona visima vinajengwa baada ya muda tatizo la maji litapungua ,kwa hiyo baada ya mwaka mmoja tutaweza kupata maji ya kutosha katika jiji letu la Dodoma kwa kweli ninaashukuru sana wizara ya Maji kwa kushirikiana na DUWASA katika utekelezaji wa miradi hii”,amesema.

Kwa upande  wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso takribani visima 10 vimechimbwa katika jiji la Dodoma huku mkakati wa maji kutoka ziwa Victoria ukiendelea.

“Watu katika jiji la Dodoma wameongezeka Mhe.Rais ametupatia Bilioni 5 kuhakikisha tunafanya maboresho ya haraka ,tumechimba visima takriban 10  ,kuna visima vikubwa 3  ambavyo tumevichimba kimoja kina uwezo wa kutoa zaidi ya lita 400,000 kwa saa  tuna tank kubwa hapa Buigiri   la lita milioni 2.5 hii yote kuhakikisha  wananchi wa Dodoma wanapata maji kwa haraka  na mkakati wa haraka tulionao ni kuleta maji kutoka ziwa Victoria”,amesema.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira jijini Dodoma Mhandisi Aron Joseph amesema mradi wa maji Buigiri Chamwino umefikia asilimia 98.

“Kama DUWASA  tunahakikisha huduma ya maji inaboreka zaidi katika jiji la Dodoma , mradi huu wa Buigiri Chamwino  ulikuwa  wa thamani ya Tsh.bilioni 2.5  lakini tumeutekeleza kwa Tsh.Milioni 998 kwa maelekezo ya wizara katika kuhakikisha tunapunguza gharama na tumefanikisha  kwa sababu tupo asilimia 98 ya  utekelezaji wa mradi ili uweze kukamilika”,amesema.

Hata hivyo, Kamati ya kudumu ya Bunge ya kilimo,Mifugo na Maji imeishauri Wizara pamoja na taasisi zake ikiwemo mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Dodoma [DUWASA]  na jiji la Dodoma kwa ujumla kuwa na mpango kabambe wa kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujenga nyumba zitakazokuwa zina miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kwa wingi ili kuondoa changamoto ya uhaba wa maji .
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger