Mwanaume aitwaye Shija Mwanzalima (30) mkazi wa Nyantorotoro mkoani Geita amejiua kwa kujinyonga baada ya kumjeruhi kwa kumchoma kisu tumboni mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea wiki iliyopita nyumbani kwa mama wa mtoto huyo Nyantorotoro.
"Chanzo cha tukio hili la kinyama ni msongo wa mawazo baada ya Shija Mwanzalima pamoja na mkewe kwenda hospitali kupima afya na kuonekana maambukizi ya VVU huku mkewe akiwa mzima licha ya kuishi pamoja",amesema.
Amesema baada ya majibu walirudi nyumbani na kumtuma mkewe dukani kununua dawa na kisha yeye kufanya unyama huo ambapo mtoto alipata majeraha makubwa na amelazwa kwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.
0 comments:
Post a Comment