Monday, 4 January 2021

MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG KITANGILI SHINYANGA ADAIWA KUPOTEA

...
 
Mchungaji Paulo Msangi wa Kanisa la TAG Kitangili mjini Shinyanga ambaye amedaiwa kupotea.
Mchungaji Paulo Msangi wa Kanisa la TAG Kitangili Mjini Shinyanga (kushoto) ambaye amedaiwa kupotea, akiwa na mke wake Beatrice Mdei,ambaye ametoa taarifa za kupotea kwake.

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog 
Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Kitangili Mjini Shinyanga Paulo Msangi, amedaiwa kupotea kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 4,2021 mke wa mchungaji huyo Beatrice Mdei amesema mume wake aliondoka Novemba 30 mwaka 2021, akiaga kuwa anakwenda Mpanda kufuata Mchele wa biashara lakini muda mfupi simu yake haikupatikana tena na mpaka sasa hawajui alipo. 

Amesema mme wake huyo mbali na uchungaji, alikuwa akifanya biashara ya kuuza mchele na kuusafirisha kwenda kwenye mikoa mbalimbali ikiwamo Arusha na Moshi, lakini tangu aange kwenda Mpanda muda mchache simu yake haikupatika na hawajui alipo mpaka sasa, huku wakiendelea kumtafuta. 

“Tumepiga simu kwa rafiki zake nao wanasema hajui alipo, na hawana mawasiliano naye, na wakimpigia simu yake haipatikani, hivyo naomba Serikali kupitia Jeshi la Polisi linisaidie kumpata mume wangu, napata shida ya kulea watoto mwenyewe na mimi sina hata kazi,”amesema Mdei. 

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Debora Magiligimba, amesema taarifa za mchungaji huyo kudaiwa kupotea wamezipata na wanazifanyia kazi.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger