Saturday, 2 January 2021

KAMATI YA FEDHA,UONGOZI NA MIPANGO YAANZA KUCHUNGUZA MAGARI YA HALMASHAURI

...

Waliovaa majoho,kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime Apoo Tindwa,kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyakonga.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya Tarime
****

Na Dinna Maningo,TARIME
KAMATI ya Fedha,Uongozi na Mipango imeanza kuchunguza magari ya halmashauri ya wilaya ya Tarime ambayo baadhi hayakuorodheshwa kwenye taarifa ya mali za halmashauri na hivyo madiwani kuagiza ufanyike uchunguzi wa utambuzi wa magari.

Kamati hiyo yenye wajumbe 12 akiwemo mbunge Mwita Waitara imeanza uchunguzi Desemba 31,2020 na itakabidhi ripoti yake Januari 11,2021 katika kikao cha baraza la Madiwani kama iliyoagizwa na Baraza la Madiwani katika kikao cha Desemba 21,2020.

Katika kikao cha Madiwani ilibainika kutokuwepo kwa baadhi ya mali za halmashauri wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime Apoo Tindwa  juu ya mali za halmashauri iliyowasilishwa mbele ya Baraza la Madiwani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyakonga Simion Samwel alisema kuwa kamati hiyo itafanya uchunguzi wa mali zote za halamsahuri ambapo wameanza na uchunguzi wa magari.

Samwel alisema kuwa taarifa ya mali iliyowasilishwa ilibainika kutokuwepo kwa baadhi ya mali yakiwemo magari,nyumba za watumishi,Jenereta huku gari lingine likiwa limeandikwa kwa namba bandia ambalo lilikuwa limefichwa.

"Kwenye ile taarifa ilionyesha kuna magari 13 na trekta moja lakini magari yaliyopo ni 18 mbali na hilo trekta pamoja na gari ambalo lilikuwa limefichwa,kuna gari SM 5142  landcluza pikapu la utawala ambalo ni namba bandia hakuna gari lenye hizo namba,gari halisi lililopo ni SM 5241ambalo lilikuwa limefichwa kwenye gereji moja" alisema Samwel.

Mwenyekiti huo alisema kuwa kutokana na utata huo alilazimika kutoa usafiri wake kwa wajumbe wa kamati hiyo na kwenda mkoani Mwanza kubaini magari yaliyoko gereji kwenye matengenezo.

"Nilisema siwezi kupokea taarifa ambayo haina ukweli bila kujiridhisha,tulikuta magari mwili moja linadaiwa zaidi ya milioni 15 na lingine zaidi ya milioni 29 yakiwemo na madeni ya nyuma tangu mwaka 2017,kamati itafatilia kujua magari yaliyopo,mazima,mabovu na kama yote yapo"alisema Samwel.

Hata hivyo mwandishi wa gazeti hili alimpigia simu Mkurugenzi wa Halmashauri Apoo Tindwa kupata ufafanuzi na sababu za baadhi ya mali kutoonekana kwenye taarifa hakuwa na mengi zaidi ya kusema;

" Wamefatilia magari yote yapo,hilo jenereta lipo isipokuwa baadhi yalisaulika kuorodheshwa na marekebisho yamefanyika"alisema Tindwa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger