Saturday, 7 November 2020

Wanafuzi waboreshewa vyoo kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

...

Samirah Yusuph.
Maswa. Kukamilika kwa ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi wilayani Maswa imetajwa kuwa ni moja ya sababu za kutokomeza magonjwa ya mlipuko wilayani hapo.
Ujenzi uliogharim kiasi cha shilingi milioni 178.7 kukamilisha matundu 125 katika shule saba za msingi  itakuwa ni msaada kwa wanafunzi na jamii katika kujilinda na magonjwa hayo kwa matumizi sahihi ya vyoo.

Ambapo mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Fedrick Sagamiko alisema ujenzi umekamilika kwa asilimia 95, mradi uliotekelezwa kupitia programu ya Afya na Elimu  shuleni (SWASH) katika awamu ya kwanza, alisema:

“Ni mradi wa benki ya dunia lakini upo chini ya usimamizi wa ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI)  mradi huo unatekelezwa katika shule ambazo zilikuwa na changamoto ya vyoo kwa wanafunzi pamoja na walimu".

Sagamiko Alizitaja shule hizo kuwa ni Jija A matundu (20), Malampaka(33), Mandang'ombe(7), Maswa(30), Mwabulimbu(15), Mwashegeshi(9) na Sangamwalugesha(11).

Katika ujenzi huo kuna mambo ya msingi ambayo yamezingatiwa ambayo ni elimu,afya na maji kwa lengo la kutunza mazingira na kuwa msafi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.

Alisema kuwa wamehakikisha vyoo hivyo vinakuwa na mfumo wa maji ili mtumiaji mara baada ya kutumia ananawa mikono na kuwa msafi na hivyo kujiepusha na aina yoyote ya magonjwa yanayotokana na uchafu na kuongeza kuwa:

"Ujenzi wa vyoo hivyo umechangiwa na wananchi wa maeneo husika huku akiwashukuru kwa kujitoa katika kushiriki na kuhakikisha vyoo hivyo vinakamilika".

Awali Afisa Elimu Msingi wilaya ya Maswa Saimon Bujimu, alihakikisha kuwa kwa ushirikiano na wakala wa maji wilayani hapo wataweza kutatua changamoto ya maji katika shule hizo ili  kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira safi na salama".

MWISHO.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger