Monday, 9 November 2020

Raia Wawili Wa Irani Wahukumiwa Kifungo Cha Miaka 30 Jela Kwa Kosa La Kusafirisha Madawa Ya Kulevya

...


Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu ‘Mahakama Mafisadi’, imewahukumu Raia wawili wa Iran kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 111.02.

Pia Mahakama hiyo imetaifisha Jahazi lililokuwa likisafirisha sawa hizo na kuamuru kuteketezwa kwa dawa hizo za kulevya.

Raia hao ambao watatumikia kifungo hicho ni Nahodha, Nabibaksh Bibade na Injinia Muhammad Hanif wa Jahazi lililokuwa likisafirisha dawa hizo, na washtakiwa wengine 11 wameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Walioachiwa ni Abdallah Sahib, UIbeidulla Abdi, Naim Ishaqa, Moslem Golmohamad, Rashid Badfar, Omary Ayoub, Tahir Mubarak and Abdulmajid Pirmuhamad, ambao ni Raia wa Iran na Ally Abdallah na Juma Amour ambao ni Watanzania.

Hukumu hiyo namba 14/2018 imesomwa na Jaji Imakulata Banzi wa Mahakama hiyo baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa mashtaka, sheria na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, wakati kesi hiyo ilipokuwa ikisikilizwa.

Jaji Banzi amesema, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya Nahodha Bidade na Injinia Hanif bila kuacha shaka lolote kwa hiyo washtakiwa wamepatikana na hatia ya kusafirisha dawa hizo kinyume na sheria.


 


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger