Tuesday, 10 November 2020

Ndugai: Hakuna Kubebana.... Ukiwa Mbunge Bubu Umekwisha

...


 Spika mteule wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amewataka wabunge waliochaguliwa na wananchi kutokaa kimya ndani ya Bunge kwani wananchi wamewachagua kwa ajili ya kuwasemea changamoto na kutafutiwa ufumbuzi.

Akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge, Ndugai amesema, wabunge wanapaswa kujua walichokifuata ndani ya Bunge na kukaa kimya sio nidhamu bali ni kutowandekea haki wananchi waliowachagua.


“Ni kweli kabisa wabunge wengi wa bunge la 12 wanatoka CCM lakini hilo halimaanishi kwamba bunge hili sasa litakuwa la ndiyo,  ndiyo,  ndiyo wala haimaanishi kwamba bunge hili litakuwa la hapana, hapana, ni bunge ambalo naamini litatekeleza wajibu wake kama ipasavyo.

“Hakuna kubebana, niwape usia wabunge wageni na wengine waliokuwepo, ukichagua kuwa mbunge bubu, usiyesema, unayejipendekeza, husemi chochote, upoupo tu, eti ili uonekane una nidhamu kwenye chama au mahali kwingine umeliwa, usidhani kwamba jambo hilo kwa wananchi wako lina tija, utakuwa umejimaliza kwa wananchi wako."Amesema Ndugai ambaye amewahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la 10 na Spika wa Bunge la 11.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger