Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kuuza na kununua Hisa kwa njia ya simu za mkononi (Hisa Kiganjani) jijini Dar es Salaam Novemba 20 2020. |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nikodemus Mkama wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na madalali wa DES wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kuuza na kununua Hisa kwa njia ya simu za mkononi (Hisa Kiganjani) jijini Dar es Salaam Novemba 20 2020. Kutoka (kulia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT), Sosthenes Kewe na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Ricco Boma. |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nikodemus Mkama (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wafanyakazi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutumia kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi katika soko la hisa Dar es Salaam Novemba 20 2020. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa (DSE), Moremi Marwa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT), Sosthenes Kewe (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Ricco Boma.
Na Robert Okanda
Tanzania leo imezindua mfumo wa kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi unaoitwa Hisa Kiganjani, hatua inayolenga kuongeza wigo wa ushiriki wa wananchi na wawekezaji katika uwekezaji kupitia masoko ya mitaji na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla.
Uzinduzi wa mfumo huo umefanywa makao Makuu ya Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama ambapo amesema uwepo wa mfumo wa kununua na kuuza hisa kwa njia ya mtandao, unatarajiwa utoe matokeo chanya katika sekta jumuishi ya kifedha, baada ya tafiti kuonyesha asilimia 60 ya Watanzania wanatumia huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi, ikiwa ni pia ni kuunga jitihada zinazoendelea za kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya kijamii kujenga utamaduni wa kuwekeza kwenye masoko ya hisa na mitaji.
Kwa mujibu wa Mtendaji huyo, Mfumo huo umeidhinishwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana baada ya kukidhi matakwa ya kisheria, vigezo na kanuni za usimamizi wa masoko ya mitaji kimataifa zinazotolewa na Taasisi ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji ulimwenguni yaani ''International Organaization for Securities Commission (IOSCO).
Bwana Mkama aliongeza kusema kwamba mfumo huo unatarajia kuwezesha kuongezeka kwa miamala katika soko la hisa na inatarajiwa kwamba ukwasi wa soko la hisa utaongezeka. 'Ukwasi Mkubwa wa soko ni kiashiria muhimu cha ubora wa soko kinachovutia wawekezaji wengi wa ndani na wa kimataifa'
Aidha Mfumo huo unatarajiwa pia kuongeza mchango katika jitihada za kuongeza uelewa na elimu ya fedha kwa umma zinazofanywa na DSE na CMSA
Alizitaja baadhi ya jitihada hizo ni pamoja na mipango na shindano la Masoko ya Mitaji kwa wanafunzi wa Vyo Vikuu na Taasisiza elimu ya juu yaani (Capital Market Universities and Higher Learning Institutions
Challenge linaloendeshwa na CMSA; na shindano la Uwekezaji kwa Wanafunzi yaani; DSE Scholar Investiment Challenge linaloendeshwa na soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na mpango wa DSE wa kuendeleza biashara yaani, DSE Enterprise Acceleration Program.
Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Bwana. Moremi Marwa, amesema mfumo huo umebuniwa ili kuongeza idadi ya wawekezaji kwenye taasisi hiyo kutoka laki tano na nusu ya sasa ambayo ni sawa na asilimia moja ya Watanzania wote lakini pia huduma za DSE kuwafikia watu wengi sehemu waliko ndani na nje ya nchi tofauti na sasa ambapo huduma hizo zinapatikana jijini DSM pekee.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Sosthenes Kewe amesema baada ya Tanzania kupata mafanikio ya kuingia uchumi wa kati, hivi sasa inaingia katika uchumi shindani unaohitaji ushiriki mpana wa jamii katika masuala ya kuinua uchumi.
|
0 comments:
Post a Comment