Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeteua majina mawili ya wanachama wake, watakaogombea Uspika na Naibu Spika wa Bunge la 12 la Tanzania.
Pia, chama hicho, kimeteua jina moja la mwanachama wa chama hicho kuwania Uspika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Uteuzi huo umefanywa na kikao cha kamati kuu ya CCM kilichokutana juzi Alhamisi jijini Dodoma tarehe 5 Novemba 2020 chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.
Walioteuliwa ni; Job Ndugai kuwa mgombea Uspika na Dk. Tulia Ackosn kugombea Naibu Spika wa Bunge la Tanzania.
0 comments:
Post a Comment