Tuesday, 3 November 2020

Atiwa Mbaroni Kwa Kumuua Mkewe na Shemeji Yake

...

Jeshi  la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mtuhumiwa Faraji Yunus (44), mkazi wa Kijiji cha Kikagati wilayani Muleba mkoani Kagera, kwa tuhumza za mauaji ya mkewe na shemeji kwa shoka.

Anadaiwa kuwaua mkewe, Nadia Coroneli (35) na shemeji yake, Shadia Yunusu (25), wakazi wa kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, alisema kuwa Oktoba 29, mwaka huu majira ya saa 12 jioni, mtuhumiwa akiwa Kijijini hapo alisababisha ugomvi uliosabanisha mauaji hayo.

Kamanda alisema, mtuhimiwa alipata taarifa kuwa mkewe alikuwa akifanya usaliti wa ndoa na kufikia hatua ya kutaka kwenda kuolewa sehemu nyingine, hivyo mtuhumiwa kuanza matukio ya kuzua ugomvi.

"Alipopata taarifa hizo alianza ugomvi na mkewe, ambao ulipelekea kumuua mkewe  Nadia na Shadia Yusuph, mke wa mdogo wake Yusuf Yunusu kwa kutumia shoka," alisema Kamanda Malimi.

Aidha, alisema akiwa katika ugomvi huo, alifika mtu ambaye ntuhumiwa alikuwa akidai kuwa ana mahusiano na mkewe, na kutaka kuamulia ugomvi huo.

Kamanda alisema mtuhumiwa alimuua shemeji yake kutokana na kumtuhumu kuwa alikuwa anamtafutia mabwana mkewe, huku akijua kuwa ni mke wake wa ndoa.

Alisema baada ya tukio hilo, mtuhimiwa alijaribu kukimbia , lakini juhudi za Polisi wilayani Muleba ziliwezesha kukamatwa na kufikishwa kituoni.

Alisema, upelekezi wa tukio unaendelea ili kubaini sababu zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger