Saturday, 2 April 2016

SERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA KUAJIRI WATUMISHI WA AFYA (AJIRA ZA AFYA 2015/16) 10000

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Serikali kuajiri watumishi wa afya 10,000

Serikali inatarajia kuajiri watumishi 10,000 wa sekta ya afya katika mwaka ujao wa fedha ili kukabiliana na upungufu wa wataalamu wa fani hiyo nchini.

Hayo yalisema jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla wakati akizindua majengo yatakayotumika kufundishia wakunga na wauguzi yaliyokarabatiwa na Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU).

Dk Kigwangalla alisema Serikali ina upungufu wa asilimia 51 ya wakunga na wauguzi na ili kukabiliana nao, imeamua kuongeza idadi ya wanafunzi katika vyuo vya afya.

“Nakipongeza Chuo Kikuu Cha Aga Khan kwa kuzalisha wataalamu wa fani ya ukunga na uuguzi kwa ngazi ya shahada na bado Serikali inahitaji kuwa na vyuo vingi vya afya ili kupunguza tatizo la uhaba wa wataalamu wa afya,” alisema.

Awali, Makamu wa Rais na Ofisa Mkuu wa Fedha wa AKU, Al-Karim Haji alisema chuo hicho kimepatiwa Sh2.9 bilioni na Benki ya Ujerumani (KFW) kwa ajili ya kukarabati vyumba na majengo ya kufundishia watalaamu hao.

“Lengo letu ni kuongeza ubora wa watumishi wa fani ya ukunga na uuguzi kwa sababu hapa nchini tumebaini kuwa kuna upungufu mkubwa wa vifaa na vyuo vya kisasa vyenye ubora wa kufundisha,” alisema Haji.

Alisema kupitia uboreshaji huo, AKU itachukua wauguzi na wakunga ambao wako kazini na kuwafundisha mara mbili kwa wiki ili waongeze ujuzi na kuwawezesha kupata shahada kwa wale wenye stashahada.

“Katika kipindi cha miaka 10, Chuo Kikuu Cha Aga Khan kimefanikiwa kuwafundisha manesi zaidi ya 600 katika ngazi ya stashahada na shahada,” alisema Haji.

Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dk Gerd Muller alisema walitoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini.

Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera alikipongeza chuo hicho kwa kuboresha sekta hiyo na mchango wake unaonyesha namna wataalamu wa afya watakavyopata elimu bora ambayo inakidhi viwango vya kimataifa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger