Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bi. Hilda Nkanda Kabisa kuwa Kamishna wa kazi.
Kabla
ya Uteuzi huo, Bi. Hilda Nkanda Kabisa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi,
Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Bi. Hilda Nkanda Kabisa, anachukua nafasi iliyoachwa na Bw. Sauli Kinemela ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amemteua Prof. Siza D. Tumbo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha
Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC).
Kabla
ya Uteuzi huo, Prof. Siza Tumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Sokoine (SUA) aliyebobea katika masuala ya Uhandisi Mitambo
ya Kilimo.
Prof. Siza Tumbo anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Evarist Ng'wandu ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria.
Uteuzi huu wa watendaji wakuu wa taasisi za serikali umeanza tarehe 26 Machi, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
01 April, 2016
0 comments:
Post a Comment