Rais Magufuli atengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne kilango Malecela kuanzia leo.
Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ana kilango
Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna
watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake
na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na
awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya
shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana
matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza
kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa
Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.
0 comments:
Post a Comment