Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa
Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi
cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169 kwa
kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Akiongea
na waandishi wa habari, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa
agizo hilo ni kufuatia agizo la Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi katika halmashauri zote ili
kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa mishahara kinyume na utaratibu za
utumishi.
Alisema
katika hao watumishi hewa 169 waliowabainika wapo ambao walishafukuzwa
kazi, wapo ambao wameshafariki na wengine hawana sifa za kuwa watumishi
wa umma.
Mhe.
Maganga alisema kuwa suala la kuwa na wafanyakazi hewa ni wizi ambao
hauwezi kuvumilika na wizi wa kuibia wanyonge hauwezi kuvumilika.
"Hakuna
anayeweza kuvumilia wizi wa waziwazi kiasi hiki unaofanywa na baadhi ya
watumishi wasiowaaminifu, wale wote watakaobainika wajiandae kwani
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao"Alisema Maganga.
Alisema
kuwa fedha walizokuwa wakilipwa watumishi hao hewa kwaajili ya
mishahara zinatakiwa kurudi zote, pia wakurugenzi wawafute watumishi hao
hewa kwenye orodha ya malipo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa sasa hivi katika serekali hii ya awamu ya tano hakuna kufanya kazi kwa mazoea.
Alizitaja
halmashauri zenye watumishi hewa kuwa ni halmashauri ya kasulu
watumishi 78,halmashauri ya Kigoma 23,Manispaa ya Kigoma Ujiji
29,halmashauri ya Buhigwe 11,Uvinza 19,kibondo 5,ofisi ya Mkuu wa Mkoa 4
na halmashauri ya Kakonko hakuna mtumishi hewa.
0 comments:
Post a Comment