Sunday, 20 March 2016

Paul Makonda Aweka Wazi Mikakati yake ya Kuubadilisha Mkoa wa Dar es Salaam, Ataka Wenye Nyumba zilizochakaa Wazipake Rangi

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezindua kampeni ya kufanya jiji la Dar es salaam kuonekana safi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko pamoja na kufanya jiji kuwa kivutio kwa wageni.

Makonda amefanya uzinduzi huo leo alipokuwa akizungumza na watendaji wa halmashauri zote za Dar es salaam katika kuwakumbusha namna ambavyo amejipanga katika kutatua kero za wananchi na kuwataka watendaji hao kuendana na kasi yake.

Kampeni hiyo ambayo inakwenda kwa jina la 'Naona Aibu' ina lenga kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi kuanzia kwenye mazingira ya majumbani hadi kwenye barabara zote za jiji.
''Hatuwezi kuwa wasafi wa mioyo kama tunaishi kwenye mazingira machafu kila mtu aseme naona aibu, ukipanda kwenye daladala ukiona uchafu sema naona aibu, ukiwa mtaani kwako sema naona aibu''. Amesisitiza Makonda katika hotuba yake ambayo imedumu kwa zaidi ya saa 3.

katika kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa, ametangaza kuanzisha shindano kwa kila mtaa, ambapo mitaa yote ya jiji la Dar es salaam itashindanishwa kwa usafi, na mtaa utakaoibuka mshindi utapata zawadi ikiwa ni pamoja na kitita cha shilingi milioni 5 kwa wajumbe wa mtaa huu.

Pia amewashauri wenyeviti wa serikali za mitaa kuwahamasisha wananchi wao kupaka rangi nyumba zao ili kupendezesha jiji kwa kuwa usafi ni pamoja na kuwa na nyumba zinazopendeza.
"Usafi ni pamoja na kupendezesha nyumba, waambieni watu wenu wapake rangi nyumba zao, zipendeze" Amesema mkuu huyo wa mkoa.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amewataka watendaji wote wa mkoa wa Dar es salaam na wanasiasa wote kutambua kwamba muda wa siasa sasa umekwisha na kilichobakia ni kufanya kazi kwa maendeleo ya wananchi.

''Wanasiasa kwenye jambo langu ukikaa mbele nitakushughulikia na wala sioni haya''- Amesema Makonda.
Hata hivyo amepiga marufuku biashara mbalimbali zinazofanyika katika maeneo ya barabara za jiji la Dar es salaam na kusisitiza kuwa biashara hizo hulikosesha taifa mapato vilevile kuweka wananchi katika hali ya hatari ya kugongwa na magari muda wowote.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger