Monday, 21 March 2016

SERIKALI YAANZA KUHAKIKI MISHAHARA HEWA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Siku chache baada ya wakuu wa mikoa kuapishwa na Rais John Magufuli, imeelezwa kuwa wakuu hao wametoa agizo la kuhakiki taarifa za watumishi wa umma kwenye mikoa yao.

Agizo hilo la Rais linalenga kubaini watumishi hewa katika mikoa na wilaya nchini. Kazi hiyo imeanza kutekelezwa kwenye baadhi ya hospitali za Serikali nchini.

Taarifa zilizoptaikana jana, zimeleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke na nyingine za mikoani, watumishi wote wametakiwa kupeleka viambatanisho kadhaa kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao za ajira.

Chanzo kutoka hospitali ya Temeke kilieleza kuwa viambatanishi hivyo ni pamoja na barua ya ajira, wasifu wa kazi na stakabadhi ya malipo ya mshahara.

Chanzo hicho kilisema kuwa agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na wafanyakazi wanatakiwa kukabidhi viambatanisho hivyo kuanzia wiki hii.

Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema, “Hatuhakiki watumishi wa sekta ya afya tu ni watumishi wote wa umma.”

Alisema watumishi ambao wako nje ya vituo vyao vya kazi, wametakiwa kurejea mara moja kwa ajili ya kazi hiyo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger