Rais John Magufuli, ambaye amejipa kazi ya “kutumbua majipu”, sasa anaweza kufanya kazi yake vizuri zaidi baada ya kukabidhiwa ripoti tano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambazo anaweza kuzitumia kama kitendea kazi.
Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli
na Serikali yake amekuwa akifanya kazi ya kuibua uozo kwenye taasisi za
Serikali, kusimamisha na kutengua uteuzi wa watumishi wa umma
wanaojihusisha na ufisadi na wakati fulani amekuwa akiitaja ripoti
iliyopita ya CAG kuwa ndiyo iliyoanika uozo anaofanyia kazi.
Jana,
“mtumbua majipu” huyo alikabidhiwa ripoti ya kwanza ya CAG tangu
aapishwe kuwa Rais Novemba 5 mwaka jana na sasa ana kitendea kazi rasmi
cha kufanyia kazi.
CAG Mussa Assad alimkabidhi Rais Magufuli
taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba
inayomtaka akabidhi ripoti hizo kwa Rais kabla ya mwisho wa mwezi Machi.
Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, kaimu mkurugenzi wa
mawasiliano – Ikulu, Rais Magufuli, ambaye aliwaomba wabunge kumpa
ushirikiano katika kutekeleza kazi za wananchi wakati akizindua Bunge
Novemba 20, atazikabidhi ripoti hizo kwenye chombo hicho ndani ya siku
saba za mwanzo za Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi na Moja utakaofanyika
mjini Dodoma kuanzia Aprili 19.
“Rais Magufuli amempongeza CAG
na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo na ametoa wito kwa chombo hicho
kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi. Ameahidi kuwa serikali
itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake,” inasema taarifa
hiyo.
0 comments:
Post a Comment