Naibu
Waziri wa Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo amesema
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya inanuka ufisadi unaofanywa
na baadhi ya wakuu wa idara.
Kauli
hiyo ya waziri inatokana na tuhuma za upotevu wa zaidi ya Sh800 milioni
mwaka 2010/2011 zilizolenga kuboresha elimu ya sekondari wilayani
Mbarali.
Fedha
hizo ambazo zinaweza kutengeneza madawati 1,600 yanayotosheleza
mahitaji ya wanafunzi 4,800, ikiwa dawati moja kwa bei ya soko kwa sasa
ni Sh50,000 zilifujwa na watumishi ambao miongoni mwao bado wapo.
Jafo
alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na wakuu wa idara, watumishi na
madiwani wa halmashauri hiyo kwenye ziara yake iliyolenga kutoa
maelekezo ya kiutendaji.
Mkurugenzi
wa halmashauri hiyo, Yeremiah Mahinya alimhakikishia Jaffo kwamba
watatekeleza maagizo waliyopewa kwa ufanisi na kwa muda, ikiwamo
kuondokana na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Mkuu wa wilaya hiyo, Gullamhusein Kiffu alisema mtumishi atakayeshindwa kutimiza majukumu vizuri atamchukulia hatua.
0 comments:
Post a Comment