INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekabidhi gari la kubebea wagonjwa
kwa hosipitali ya wilaya ya Chalinze, Ikiwa ni utekelezaji wa ilani
na ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa wananchi ikiwa ni
pamoja na wa jimbo la Chalinze.
Gari hilo la kubebea wagonjwa limekabidhiwa kwa niaba ya Rais, na
Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo, Katibu Mkuu Ikulu
Ndugu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Mheshimiwa Rais kwa
hosipitali hiyo ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi
ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuboresha huduma ya afya kwa
wananchi wake kote nchini.
Aidha, Ndugu Ilomo amewaomba viongozi wa jimbo la Chalinze kulitumia
gari hilo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi wa eneo
hilo.
Akipokea gari hilo kwa niaba ya wananchi wa jimbo na Wilaya ya
Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete
amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada huo
na kuahidi kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kusema
kuwa, utendaji kazi wa Rais Magufuli umekuwa ukiungwa mkono na wananchi
wa kada mbalimbali na kuwaomba watanzania kuzidi kumuombea kwa Mungu.
Kwa upande wake Dakta Nasoro Ally Matuzya, amesema gari hilo limekuja
kwa wakati muafaka kwa kuwa umezingatia utekelezaji wa malengo ya
Milenia hususan lengo namba nne linalosisitiza kupunguza vifo vya mama
wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze Ndugu Saidi Omar
Zikatimu amesema gari hilo la kubebea wagonjwa litakuwa msaada mkubwa
kwa wananchi wa jimbo hilo la Chalinze hususan katika kusaidia kutoa
wagonjwa ambao wako katika maeneo ya vijijini wilayani humo na
kuwafikisha katika hospitali ya Chalinze na hivyo kunusuru maisha yao
kwa kupata huduma za afya kwa haraka.
Mbali na Wilaya ya Chalinze kupata msaada wa gari hilo la kubebea
wagonjwa, tayari magari mengine mawili ya kubebea wagonjwa
yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu mkoani
Morogoro.
Hospitali mpya ya Wilaya ya Chalinze imepanda hadhi kutoka kituo cha
Msoga ambayo ilikuwa haina gari la kubebea wagonjwa na hivyo kufanya
usafirishaji wa wagonjwa kutoka hospitali hiyo hadi hospitali ya rufaa
ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi au kutoka maeneo ya vijijini kuwa mgumu.
Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu
18 Machi 2016.
0 comments:
Post a Comment