Jeshi
la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata jumla
ya watu 287 ambao ni dada poa pamoja na kaka poa katika operation maalum
iliyofanyika maneo mbalimbali ya Jiji hilo.
Operation
hiyo ilitangazwa na kamishna wa kanda maalum mnamo Tarehe 7 mwezi wa 3
na kuazimia kuwakamata madada poa na makaka poa pamoja na wateja wao
ambao watakutwa wakiwanunua.
Katika
mkoa wa kipolisi wa ilala operation hii imefanikiwa kuwakamata jumla ya
madada poa 51 kutoka katika maeneo mbalimbali yakiwemo
msimbazi,Buguruni,na stakishari,pia imewakamata jumla ya makaka poa 12
ambapo 11 wanatokea Buguruni na mmoja kutoka msimbazi.
Mkoa
wa kipolisi wa temeke umefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa
22,ambapo changombe walipatikana 12,na mbagala walipatikana madada poa
10.
Aidha
katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni operation hiyo imefanikiwa
kuwakamata madada poa 76 kutoka maeneo ya osyterbay madada poa
49,magomeni 23,na kawe madada poa 4,pamoja na makaka poa 4.
Akizungumza
na wanahabari jana makao makuu ya polisi kanda maalum ya Dar es salaam
,Kamishna wa kanda hiyo CP Simon Sirro aliwataka watu wenye tabia kama
hizo kuacha mara moja kwani ni kinyume na mila na desturi za mtanzania
ambapo amewataka kutafuta biashara nyingine halali za kufanya.
0 comments:
Post a Comment