Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu amewataka
watu wote wanaopindisha sheria, majambazi na wahalifu wote kutafuta kazi
nyingine halali za kufanya.
Meja
Kijuu aliyasema hayo baada ya kula kiapo cha utiifu na uadilifu
kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Kagera mkoa ambao upo pembezoni mwa nchi
unaokabiliwa na matukio ya mara kwa mara ya uhalifu.
''Namshukuru
Mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyonayo kwangu na nitafanya kazi kwa
kuzingatia yale ambayo ameyasema na kuhakikisha maendeleo
yanapatikana''-Amesema Meja Kijuu
''Sitakubali
watu wazurure hovyo na kuacha kufanya kazi za uzalishaji na
nitahakikisha napambana na wahalifu wote kwa uwezo wote nilionao"-Amesisitiza Meja Kijuu.
Aidha
Rais Magufuli aliwaapisha wanajeshi wastaafu Meja Jenerali Mstaafu,
Ezekiel Elias Kyunga, aliyekuwa Chuo cha Kamanda na Unadhimu (JWTZ)
ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Jenerali Mstaafu Salum Mustafa
Kijuu, aliyekuwa Mkuu wa Kamandi ya Nchi Kavu ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Wengine
ni Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa(JKT) sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Brigedia Jenerali
Mstaafu Emmanuel Maganga, aliyekuwa Makao Makuu ya Jeshi sasa ni Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma lengo la Rais kuweka wanajeshi katika mikoa ya pembezoni
ni kuleta usalama na kuimarisha amani katika mikoa hiyo.
0 comments:
Post a Comment