MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washtakiwa 17 kati ya 35
wanaokabiliwa na kesi ya kuchoma moto Kituo cha Polisi Bunju ‘A’ baada
ya Upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka
Hukumu
hiyo imetolewa mahakamani hapo na Thomas Simba, Hakimu Mkazi huku
upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Hellen Moshi, Wakili wa Serikali.
Katika
kesi hiyo, Hakimu Simba amesema hatua hiyo inatokana na upande wa
mashtaka kufunga ushahidi wao wakiwa na mashahidi 17 pamoja na vielelezo
19.
Amesema,
kutokana na kushindwa kuthibitisha mashtaka kwa washtakiwa 17 mahakama
imeamua kuwaachia huru kwa kuwa hawana hatia, huku washtakiwa waliobaki
18 wakipatikana na kesi ya kujibu.
Washtakiwa
walioachiwa ni Halifan Mshengeli, Patrick Elias, Jacob Kasambo, Amos
Machaka, Hamis Mohamed, Elia Nalomba, Juma Kapanga,
Wengine
ni Josephine Machimo, Shadya Ismail, Aisha Husseion, Jenerose Urio,
Suzan Shaulin, Mariam Mwinyi, Madgalena Nashokigwa, Mariam Rashid, Pili
Ally na Said Mwindi.
Washtakiwa
ambao wamepatikana na hatia baada ya kutolewa kwa ushahidi ni Yusuph
Sungu, Juma Koza, Rashid Liwima, Mrisho Majaliwa, Hamis Ndege, Seleman
Gwae, Baraka Nkoko, Mang’ enya Mang’enya.
Wengine
ni Abuu Issa, Ramadhan Said, Rajab Ally, Ally Athuman, Abraham Nunge,
Amina Matipwili, Mariam Hoza, Rehema Juma, Gudila Temba, Veronica
Ephraem (Mama Wambura).
Hakimu
Simba amesema, washtakiwa hao wamepatikana na kesi ya kujibu katika
mashtaka sita yanayowakabili, hivyo kutokana na wingi wa wananchi kesi
hiyo itasikilizwa siku mbili mfululizo kuanzi Machi 29 hadi 30, mwaka
huu kwa ajili ya kujitetea.
Baada
ya kusema, hayo kuliibuka hoja za kisheria kati ya Wakili Moshi na
wakili wa utetezi Felix Nkongwa kuhusu kupata dhamana kwa washitkiwa
waliobaki.
Kutokana
na mvutano wa hoja, Hakimu Simba amesema uamuzi wa kupata ama kutopata
dhamana kwa washitakiwa hao utatolewa Machi 22, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment