Mgomo wa Madereva umeanza rasmi leo katika maeneo mbalimbali nchini kama ambavyo muungano wa madereva wa vyombo vya usafiri waliahidi wakidai kutotatuliwa kero zao na serikali.
Sababu
kubwa ya madereva hao kugoma ni kuishinikiza serikali kuweka
mfumo mzuri wa ajira na kupinga kanuni inayowataka kurudia
kusoma katika chuo cha taifa cha usafirishaji,NIT kila leseni
zao zinapokwisha muda.
Madereva
hao wanadai malalamiko yao makubwa ni kitendo cha Serikali
kuongeza kifungu kidogo katika sheria mpya ya mwaka 2015 namba
31 inayowataka madereva wote wenye leseni za madaraja
E,C1,C2,C3 na C kurudi darasani kila baada ya miaka mitatu
kuongeza utaalamu katika fani hiyo ya udereva ili kupunguza
ajali za mara kwa mara zinazotokea.
Umati
wa abiria wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Darajani-Ubungu huku
kukiwa hakuna daladala yoyote inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo
wa madereva wa Daladala jijini Dar.
Baadhi
ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana kwa
daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika
kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia
na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.
0 comments:
Post a Comment