Watu wawili akiwemo jambazi mmoja na askari mwanafunzi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wamekufa na wengine kunusurika kuuawa katika tukio lililotokea juzi, mjini Mafinga mkoani Iringa wakati majambazi wakirushiana risasi na askari wa Jeshi la Polisi.
Risasi
hizo zilipigwa wakati Polisi hao wakijaribu kuokoa fedha za
mfanyabiashara Salama Semwaiko zilizoporwa na majambazi wawili
waliotumia pikipiki wakati wakifanya uporaji huo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema mfanyabiashara
huyo aliporwa fedha hizo juzi majira ya saa 2.45 asubuhi alipokuwa
akitoka nyumbani kwake kwenda kwenye biashara zake.
Tukio
hilo la kusikitisha lililovuta hisia za watu wengi na kufanya baadhi
kuzimia wengine kukimbia hovyo na kujifungia ndani kwa ajili ya kuokoa
maisha yao lilitokea katika eneo la Kinyanambo B, nje kidogo ya mji wa
Mafinga.
Kamanda Mungi alisema; “mfanyabiashara
huyo akiwa katika gari lake akielekea kwenye biashara zake mjini
Mafinga, mfanyabiashara huyo alisimamishwa na mtu mmoja aliyekuwa amevaa
koti jeusi na baada ya kusimama alimtolea silaha na kumtaka atoe fedha
na vitu vyote vya thamani alivyokuwa navyo .”
“Baada
ya kuona hana msaada mfanyabiashara huyo alijikuta akilazimika kutoa Sh
700,000 alizokuwa nazo, simu ya mkononi na baadaye ilitokea pikipiki
ambayo haikufahamika namba za usajili na kumpakia mtu huyo na kuanza
kukimbilia eneo la Kinyanambo,” alisema.
Alisema
mara baada ya majambazi hao kutoweka, Jeshi la Polisi lilipewa taarifa
na kuwahi eneo la tukio na kwa kushirikiana na wananchi walianza
kuwakimbiza majambazi hao na ndipo majibizano ya risasi yalipoanza.
Katika
hekaheka hiyo, Kamanda Mungi alisema Said Ngudi (25) ambaye ni askari
wa JKT Makutupora, Dodoma alipigwa risasi na kufa papo hapo wakati
akisaidia kupambana na majambazi hao.
0 comments:
Post a Comment