Naibu
Waziri wa Maji, Amosi Gabriel Makala,
hivi karibuni akijaribu bila
mafanikio kupiku mafanikio ya Chadema ilivyojikita kaika Kiwanda cha
Sukari Mtibwa, huku akitizamishwa mabango ya alikuwa wapi tangu mwanzo,
kushughuliki mgogoro wao na mwekezaji wa kiwanda hicho, pale wafanyakazi
walipgoma kufana kazi hadi walipw mishaara yao. Picha na Bryceson
Mathias
Na Bryceson Mathias, Movomero.
DIWANI wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Mtibwa wilaya ya
Mvomero, Luka Mwakambaya, amembana kwenye Kona na kumyima Usingizi Naibu
Waziri wa Maji na Mbune wa Jimbo hilo, Amosi Makala, kiasi cha kumfanya
ahofie Ubunge wake 2015 na kuamua kumshitakia Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda; Chadema wakidai hilo ni change la Macho.
Hofu ya
Makala inatokana na Kijiji na Serikali ya Mji Mdogo wa Madizini anaokaa,
kunyakuliwa na Chadema wakiwemo Viongozi wenzake wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) wilayani humo, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri Mvomero,
Mwenyekiti wa CCM na Katibu Mwenezi, kuongozwa na Chadema.(P.T)
Makala
akiwa bungeni hivi karibuni alimlalamikia Pinda hatari ya kupoteza jimbo
hilo kwa upinzani, pale alipofanikiwa kuwakokota Viongozi wa Chama cha
Wafanyakazi Mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU), Wakulima wa Miwa ya
nje MOA na TUCCOPRICOS, wanaotofautiana na Mwekzaji waKiwanda cha Sukari
Mtibwa, asiyewalipa malipo yao, wakitaka Mwekezaji mpya.
Katika
msafara huo ambao Diwani Chadema alitengwa, CCM kiliwapiga Changa la
Macho Wafanyakazi na Wakulima hao bila kuwapa majibu kama kitamng'oa
mwekezaji huyo kama walivyopendekeza, bali walimkumbatia Mwekezaji huyo,
anayedaiwa Mishahara ya Miezi Mitatu na Wafanyakazi, ikidaiwa Wakulima
wanadai Bil. 1.270/-, amelipa Mil.150/- tu!.
Habari
zilizonaswa toka kwenye Kikao hicho zinadai, licha ya Wakulima na
Wafanyakazi kutoa Kero Sugu za Mwekezaji huyo, Pinda alikiri kuzifahamu
na kuzisikia mara kadhaa, lakini inadaiwa alisema, hana jibu la haraka,
ila anaandaa Kikao na Mawaziri husika wa Viwanda, Kilimo na Mwanasheria
Mkuu, ichunguzwe Mikataba yake.
Aidha
inadaiwa alisema, ataandaa Ziara Maalum kwenye Viwanda vya Sukari
Kilombero, Kagera, TPC na Mtibwa, ili Mawaziri husika na wanasheria
Mkuu, Waweze kuona nini kifanyike kama Mikataba hiyo iko fyongo au
kiwete inayowaumiza.
Mwenyekiti
wa TPAWU Tawai la Mtibwa, Dominick Bayogire Mbasha, alipoulizwa ukweli
wa safari yao kwa Pinda alikiri kuwa, Majibu waliyopata hayana Mashiko
wamepigwa Changa la Macho na kwamba safri hiyo ilikuwa ya Kisiasa, na
kwamba familia zao zitaendelea na shida.
Tuliopigwa
Changa la Macho katika Msafara huo si mimi tu ni pamoja na Katibu wa
TPAWU Taifa, Mwenyekiti wa TPAWU Mtibwa, Mbasha, Mwenyekiti, Mjumbe wa
TPAWU Mtibwa, Waziri Mdemu, Katibu wa Mbunge, Jumanne Kombo, na
Wenyeviti wa Wakulima wa Miwa ya nje MOA na TUCCOPRICOS, walitoa Hoja ya
kutkaka Mwekezaji mpya haraka kama Wafanyakazi, au kijengwe Kiwanda
kingine.
Wakati
tunaenda mitamboni, tayari Wakulima wa Nje wa Kiwanda cha Mtibwa,
wamefunga Mageti ya Kiwanda cha Mwekezaji, kutokana na ahadi ya
kuingiziwa fedha kwenye Akaunti ya Vyama hivyo vya Wakulima, ambapo hata
Kampuni ya Usafirishaji Miwa ya KIOMA inadai Mil.440/-, huku
wakikasirishwa na taarifa za Safari ya Dodoma.
Chanzo:http://chademablog.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment