Askofu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima akihubiri akiwa amekaa
katika kiti cha magurudumu kwenye ibada ya Pasaka jana katika viwanja
vya Tanganyika Packers Dar es Salaam. Picha na Said Khamis
Askofu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alihubiri akiwa katika
kiti cha magurudumu na kusema hawezi kuwatupa Mbunge wa Monduli (CCM),
Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwa kuwa ni
marafiki zake wa siku nyingi.
Pia
askofu huyo, amewataka waumini wote wa kanisa hilo kufika katika Kituo
Kikuu cha Polisi, Alhamisi ijayo siku ambayo atakwenda kukamilisha
mahojiano dhidi ya tuhuma za kumtukana Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar
es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo.
Akihubiri
mamia ya waumini waliofika kanisani hapo kwa ajili ya ibada ya Pasaka
jana, Gwajima alisema kumekuwa uvumi kwamba kuhojiwa kwake na polisi
kulitokana na kuwakaribisha wanasiasa hao kanisani kwake kwa nyakati
tofauti na kuzungumza na waumini wake.(P.T)
Alisema
alifahamiana na Lowassa tangu mwaka 1996 wakati huo mbunge huyo akiwa
Waziri wa Ardhi na tangu kipindi hicho amekuwa mtu wake wa karibu.
Alisema
alifahamiana na Dk Slaa tangu mwaka 1994 kabla hajagombea nafasi ya
urais kupitia Chadema na kwamba tangu wakati huo amekuwa rafiki wa
familia.
"Hawawezi
kunichagulia marafiki, hawa ni watu wangu wa karibu hata kabla hawajawa
na ndoto za kugombea urais, nitaendelea kuwa nao karibu," alisema.
Asimulia mahojiano
Akizungumzia
mahojiano yake na polisi, Gwajima aliwaeleza waumini wake kwamba mambo
mengi aliyohojiwa hayakuhusiana na suala la kumkashifu Kardinali Pengo.
"Polisi
walinihoji mambo mengi binafsi yanayonihusu mimi na hayakuhusiana kabisa
na Pengo, maswali ya Pengo yalikuwa machache sana," alisema.
Hata
hivyo, Gwajima alisema hana ugomvi na polisi wala Serikali kwa kuwa
amekuwa akitoa ushirikiano kwa vyombo hivyo. Akitoa mfano, alisema
Februari mwaka huu alipeleka barua polisi kueleza anataka kudhamini
kampeni kwa ajili ya kupinga mauaji ya albino kwa kushirikiana na jeshi
hilo.
"Niliwaeleza
kwamba tungezunguka na polisi mikoa yote Tanzania na wamenijibu kwamba
nipeleke ratiba ya shughuli hiyo ili tuanze," alisema.
Alisema
pia alidhamini mafunzo ya ulinzi shirikishi kwa vijana 400 kwa
kushirikiana na polisi... "Shughuli hizi zinaonyesha kwamba sina ugomvi
na polisi, bali nimekuwa rafiki kwa kushiriki katika shughuli zenye
masilahi kwa Taifa."
0 comments:
Post a Comment