Wednesday 23 January 2019

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 23,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 23, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

SH 66.6 BILIONI ZAPITISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO 2019/2020 MULEBA

Na Mwandishi wetu Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera leo hii limepitisha makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 jumla ya Mapato ya kiasi cha Sh 66.6 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ya halmashauri hiyo. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Chrisant Kamugisha amewasihi wataalam kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha mpango na bajeti iliyopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani mapato yanakusanywa kwa asilimia 100 na hata kuvuka malengo. Amesema katika Mchanganuo wa mapato hayo Mapato ya ndani yatakuwa…

Source

Share:

MTOTO MWINGINE AUAWA NJOMBE,SIMANZI YATANDA KWA WANANCHI .

Na.Mwandishi wetu Wananchi mjini Njombe wameiomba serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usalama kudhibiti vitendo vya mauaji ya watoto wa umri kati ya miaka 4-9 ambavyo vinatajwa kuongezeka tangu mwezi desemba mwaka jana na kuendelea kutishia hali ya usalama mjini humo. Wananchi hao wametoa rai hiyo baada ya mwili wa mtoto mwingine wa jinsia ya kiume kuokotwa kando ya msitu wa asili wa nundu ulioko nje kidogo ya mji wa njombe. “Ni kweli kuna mtoto mwingine amekutwa amefariki pale msituni, tulipofika pale tulitoa taarifa kwa polisi wa kituo cha Uwemba…

Source

Share:

Tuesday 22 January 2019

USAIN BOLT ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

Usain Bolt amethibitisha kuwa amestaafu kucheza soka baada ya kushindwa kupata mkataba katika klabu ya Central Coast Mariners ya Australia aliyokuwa akifanya majaribio.

''Maisha ya michezo sasa basi, sitaki kusema sikutendewa vyema lakini kwenye maisha tunaishi na tunajifunza pia, kwahiyo nina mambo mengi nitakwenda kuyafanya kwasasa ila kuhusu michezo imetosha'', amesema.

Bolt, ambaye alishinda medali za dhahabu katika mbio za Olimpiki huko Beijing, London na Rio, ameweka wazi kuwa mwelekeo wake wa sasa ni kuendeleza biashara.

Oktoba 12, 2018 Bolt alifunga mabao 2 kwenye mechi yake ya kwanza kucheza ambayo ilikuwa ya kirafiki kati ya Central Coast Mariners na Macarthur South West.

Bingwa huyo mara 8 wa Olimpiki alistaafu mbio mwaka 2017 kwenye mashindano ya Olimpiki ya London, ambapo alipata medali moja ya dhahabu na tatu za shaba huku akishika nafasi ya 3 katika mbio za mita 100.
Share:

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA MSIMU WA 16 KURINDIMA FEBRUARI 7-10 ZANZIBAR.

Na.Mwandishi wetu. BUSARA Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha kubwa la muziki la Sauti za Busara ambalo ni la msimu wa 16 linatarajiwa kurindima kwenye viunga vya Ngome Kongwe Zanzibar kwa kushuhudia shoo 44 kutoka kwa wanamuziki wa hapa nchini na Ukanda wa Afrika. Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf’ amebainisha kuwa mambo kwa sasa yamepamba moto na maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo watu mbalimbali wajiandae kufika kulishuhudia. “Wadau na wapenzi wa muziki kutoka sehemu mbalimbali…

Source

Share:

DC MJEMA APOKEA JENGO LA OFISI YA WALIMU KUTOKA SERIKALI YA JAPAN LENYE THAMANI YA DOLA ZA MAREKANI 94.5.

Na Heri Shaban MKUU wa wilaya ya Ilala sophia Mjema amekabidhiwa jengo la ofisi ya Walimu lenye thamani ya dola za Marekani 94.5 kutoka Serikali ya watu wa Japan pamoja na madarasa matatu Kwa ajili ya Shule ya Msingi Gogo iliopo Zingiziwa Wilayani Ilala. Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salam jana ambapo Balozi wa Japan nchini Tanzania Shinichi Goto alimbidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala. Akipokea msaada huo wa jengo la Utawala Shule ya Gogo Sophia Mjema alipongeza Serikali ya Japan kwa Ushirikiano wao kusaidia kuunga mkono jitihada zinazofanywa na…

Source

Share:

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AMPONGEZI MAGUFULI KUHUSU URASIMISHAJI ARDHI KWA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA MAENEO YA HIFADHI.

Na.Mwandishi wetu. Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga ampongeza Mhe.Rais John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua kwa kuruhusu baadhi ya vijiji vilivyokuwa kwenye Hifadhi ya Taifa vyenye watu wengi vibaki na kwa upande wa vijiji vingine ambavyo vimesajiliwa kimakosa wakati vipo kwenye Hifadhi Wizara tatu husika ziweze kuwajibika katika maeneo husika yaliyopo kwenye Hifadhi . Mhe.Odunga “Ningependa kuomba ushirikiano kwa Wizara husika tatu ikiwemo Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi zije ili tuweze kukaa kwa pamoja na Kamati ya…

Source

Share:

RAIS MAGUFULI AMTAKA BITEKO ASIANGALIE SURA YA MTU.. " UTAZIKWA PEKE YAKO"


RAIS John Magufuli amemtaka Waziri wa Madini, Dotto Boteko atekeleze majukumu yake bila kujali sura ya mtu kwa kuwa kaburini atakwenda peke yake.

Amesema, hasiti kumfukuza Waziri wa Madini hata kama ameiongoza Wizara hiyo kwa wiki moja.

Amewataka viongozi wa Wizara hiyo wachukue hatua, wawahamishe wataalamu wizarani na atashangaa kama hilo halitafanyika.

Ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua mkutano wa mashaurino wa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuufunga kesho.

Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Madini Dotto Biteko awe mkali, na kwamba, aliyepita, Angellah Kairuki hakuwa mkali ndiyo maana kampeleka akapumzike Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kairuki ni Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

Rais Magufuli amemuagiza Waziri Biteko, Naibu wake, Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Amos Msanjila hiyo ndani ya mwezi mmoja wawe wameweka kamera kwenye ukuta wa Mirerani na wasipofanya hivyo wajiandae kuondoka.

Via Habarileo
Share:

WAZIRI AGOMA KUTUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema hayupo tayari kutimuliwa na Rais John Magufuli kwa kushindwa kupeleka huduma za maji kwa wananchi.

Kauli ya Aweso imetokana na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya maji katika wilayani Kisarawe mkoani Pwani licha ya bajeti iliyopo.

Akizungumza leo Jumanne Januari 22, 2019 wakati wa ziara ya kikazi katika wilaya hiyo, Aweso amesema Rais Magufuli alipomteua alimpa jukumu la kuhakikisha maji safi na salama yanawafikia wananchi wote.

Kauli hiyo ya Aweso imetokana na kusuasua kwa miradi ya maji wilayani humo huku mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo akisema imeshindwa kuendelea kwa kukosa huduma ya maji.

"Tulipoteuliwa katika nafasi hizi Rais alisema anatupa wizara hii ili wananchi wapate maji na wasipopata basi atatumbua na mimi sipo tayari kutumbuliwa," amesema Aweso.


Na Cledo Michael, Mwananchi
Share:

KKKT NJOMBE SASA RUKSA KUUZA VIWANJA, ASKOFU MENGELE ATUMA SALAMU KWA WALIOKWAMISHA ZOEZI

Na Amiri kilagalila Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania kanda ya nyanda za juu kusini limejipanga kuendelea na zoezi la uuzaji wa viwanja vinavyomilikiwa na kanisa hilo mkoani Njombe kutokana na maagizo ya kusitishwa uuzaji wa maeneo hayo lilitolewa na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi alipokuwa mkoani Njombe siku chache zilizopita Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini Njombe Isaya Japhet Mengere amesema kuwa serikali kupitia wizara ya ardhi nyumba na makazi imeruhusu zoezi la uuzaji viwanja katika eneo linalojengwa chuo kikuu mjini Njombe…

Source

Share:

KK SHARKS WAICHAPA YANGA 3 - 2

Mlinda  mlango namba moja wa Yanga, Klaus Kindoki amekubali kuokota mipira mara mbili nyuma ya nyavu katika mchezo wa michuano ya SportPesa Cup ambao umechezwa Uwanja wa Taifa.

Yanga amecheza na KK Sharks ya Kenya na Kindoki amegeuka mara tatu baada ya kuanza mapema dakika ya 12 kuokota mpira nyuma ya wavu na kufanya hivyo dakika ya 36.

KK Sharks wamerejea kipindi cha pili wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0 ambayo wameyapata katika kipindi cha kwanza baada ya kushambulia sana lango la Yanga.

Kipindi cha pili dakika ya 87 Yanga wakapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Amiss Tambwe na dakika ya 90 bao la pili kupitia kwa Makambo.

KK Sharks nao wakafanikiwa kufunga bao la 3 dakika ya 90.


Share:

NDEGE YAPOTEA ANGANI..YUMO MSHAMBULIAJI MPYA WA CARDIFF CITY


Mchezaji Sala ambaye alikuwa kwenye ndege hiyo.

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Cardiff City Emiliano Sala, amepotea angani kwenye ndege binafsi jana jumatatu jioni wakati anatoka mjini Nantes, Ufaransa kuelekea Cardiff, Wales.

Mamlaka ya anga ya Ufaransa imethibitisha ndege hiyo kupotea ambapo muargentina huyo mwenye miaka 28 alikuwepo pamoja na mtu mwingine wa pili.

Sala alisajiliwa kwa ada ya rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 15 siku ya Jumamosi na alikuwa ni miongoni mwa watu wawili waliokuwepo kwenye ndege hiyo iliyopotea.

Baada ya kusaini mkataba siku ya Jumamosi, Sala alirejea nchini Ufaransa kuwaaga wachezaji wa timu yake ya zamani ya Nantes, na baadaye kuweka picha akiwa na wachezaji hao katika Instagram akiandika “ Kwa heri ya mwisho “ kabla ya kupanda ndege kurejea Wales.

Afisa anayehusika katika kuitafuta ndege hiyo John Fitzgerald anasema kuwa hatarajii kumkuta mtu yoyote akiwa hai.

“Kuna bahati ya asilimia 5 tu ya kuwapata Sala na rubani, “alisema Fitzgerald.‘ Maji ni ya baridi sana kwa sasa , kwa hiyo kama kuna ambaye amepona kwenye maji , ni baridi sana , ni saa moja tu unaweza kuwa mzima katika kipindi hiki cha mwaka‘ .

Familia ya mchezaji huyo ipo nchini Argentina na baba wa mchezaji huyo Horacio amesema alijisikia vibaya sana baada ya kupata taarifa za kupotea kwa mwanae.
Share:

OLE GUNNA SOLSKJAER NA UNAI EMERY KUKUTANA IJUMAA HII EMIRATES FA CUP


Raundi ya 4 ya michuano ya Emirates FA CUP, kuanza kupigwa Ijumaa hii ambapo kwa mara ya kwanza Ole Gunna Solskjaer na Unai Emery wanakutana, ni katika pambano la FA Emirates Cup, Je ni kocha gani kuanza kuandika rekodi ya ushindi dhidi ya mwenzie?

Share:

AZAM FC NA SIMBA FEBRUARI 22 NA YANGA APRILI 29 UWANJA WA TAIFA

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imepanga ratiba za mechi za viporo za Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, itakazocheza dhidi ya Simba na Yanga zilizotakiwa kufanyikwa kwenye raundi ya kwanza.

Ratiba hiyo mpya inaonyesha kuwa Azam FC itacheza mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Simba msimu huu, Februari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku ile na Yanga ikipigwa Aprili 29 mwaka huu.

Mechi nyingine mbili za viporo za Azam FC, dhidi ya Mbeya City na Ndanda, ilizotakiwa kucheza kwenye raundi mbili za awali za mzunguko wa pili wa ligi hiyo, itakipiga na City Aprili 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, kabla ya kusafiri hadi mkoani Mtwara kumenyana na Ndanda Aprili 18.

Katika mabadiliko hayo ya ratiba inaonyesha kuwa, msimu wa ligi utafungwa Mei 26 mwaka huu kwa mechi zote kupigwa huku Azam FC ikitarajiwa kufunga pazia hilo kwa kumenyana na Yanga, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wiki hii Azam FC inatarajia kukamilisha raundi ya 24 ya ligi kwa kucheza na Biashara United, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Ijumaa hii saa 1.00 usiku, kabla ya kuhamishia nguvu kwenye Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ikitarajia kukipiga na Pamba kwenye dimba hilo Januari 28 mwaka huu saa 1.00 usiku.

Azam FC hadi sasa imeonekana kufanya vizuri kwenye msimu huu wa ligi, ikiwa ni miongoni mwa timu zinazopigana vikumbo kuwania taji hadi sasa ikiwa nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia pointi 44 ikizidiwa pointi tisa na Yanga iliyo kileleni, lakini matajiri hao wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Share:

HATIMAYE MAKAMANDA WALIOTENGULIWA NA KANGI LUGOLA WAONDOLEWA



Share:

SHUWASA YATOA KALENDA ZA 2019 KWA WAANDISHI WA HABARI MANISPAA YA SHINYANGA

Ofisa Mahusiano ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), Nsianel Gelard ( wa kwanza kulia)  akimkabidhi Kalenda za mwaka 2019 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC),Kadama Malunde kwa ajili ya Waandishi wa Habari waliopo katika Manispaa ya Shinyanga katika ofisi ya SPC leo Jumanne Januari 22,2019. Picha na Malaki Philipo - Malunde1 blog
Kulia ni Ofisa Mahusiano ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), Nsianel Gelard akimkabidhi Kalenda za mwaka 2019 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC),Kadama Malunde
Zoezi la makabidhiano ya kalenda likiendelea. Wa kwanza kulia ni Ibrahim  Mwita kutoka SHUWASA,Wa pili kutoka kushoto ni Mweka Hazina wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC), Stella Ibengwe.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC), Kadama Malunde akiwa ofisini baada ya kupokea kalenda kutoka SHUWASA
Share:

KAKOBE: TANZANIA ILIKUWA IKIISHI NA LAANA

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe amedai Tanzania ya zamani ilikuwa ikiishi kama nchi yenye laana kutokana na baadhi ya rasilimali zake kutumika zaidi na wageni na kushindwa kuwafaidisha watanzania wenyewe.

Askofu Kakobe ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa wadau wa uchimbaji na wafanyabiashara ambapo walizungumza na Rais John Pombe Mgufuli ili kuhakikisha sekta hiyo inainua uchumi wa Tanzania.

 “lakini ni jambo la kushukuru kwa sababu Mungu amemuinua shujaa Rais Magufuli ambaye amekataa kwamba tuachiwe mashimo na urithi wetu wachukue mataifa mengine na suala hili linahitaji ushujaa sana,”  Askofu Kakobe alisema,.

 “hata Biblia inasema tutangulize yaliyo mema hata kama una hasira naye, hata Yesu Kristo alipokuwa anatoa ujumbe kwa makanisa saba alikuwa anaanza kupongeza mazuri hata kabla ya kuinua jambo lolote la kupinga, atakayekuwa anapinga atakuwa ni mkorofi na hata ukiwa na hoja itakuwa ngumu kusikilizwa,ameongeza Askofu Kakobe.

“Mimi nafikiri unapoanza kupambana na suala hili, uanze kufanyia kazi kwanza fikira za mtu. Kadiri tunapozidi kutamka vitu vizuri ndiyo tunazidi kuvichochea,” aliongeza Kakobe.

Chanzo:Eatv
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger