INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ajira kwa Wahitimu Elimu ya Juu Mwaka 2014
Katika
mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kuajiri
wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu wa mwaka 2013/2014. Ili kutekeleza
azma hii waombaji watajaza kikamilifu na wataambatanisha vivuli vya
vyeti vyao na kutuma Makao Makuu ya Polisi kwa njia ya Posta kabla ya
tarehe 31.08.2014 kwa anuani ifuatayo:
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM
Waombaji wawe na taaluma zifuatazo:
Shahada:
Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala katika Utumishi wa Umma,
Uchumi, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Usimamizi wa Sheria na
Utekelezaji[BaLE], Sheria, Ualimu, Maendeleo ya Jamii, Uandishi wa
Habari, Uandishi wa Habari za Michezo, Mawasiliano ya Umma, TV &
Redio Production, Michezo, Ugavi[BA in Procurement & Supplies],
Mawasiliano ya Redio[Bsc in Radio Communication], Mazingira[BA in
Environmental Disaster Mgt], Uhandisi Mitambo, Uhandisi Madini[Mining
Engineering], Uchoraji[BA in Fine Arts], Fedha na Benki[Finance &
Banking], Daktari[Medical Doctor] na Daktari wa Meno[Dental Surgeon],
Mkemia, Bailojia[Molecular Biology].