Tuesday, 29 April 2025

WAZIRI MKUU : SERIKALI ITAENDELEA KULINDA UHURU WA HABARI KWA VITENDO, WAANDISHI TUMIEMI AKILI MNEMBA KWA UWAJIBIKAJI

...

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza jijini Arusha leo Aprili 29, 2025 wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza jijini Arusha leo Aprili 29, 2025 wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza jijini Arusha leo Aprili 29, 2025 wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani

***

👉Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Asisitiza Akili Mnemba Isaidie, Isiwe Kikwazo kwa Uhuru wa Habari 

👉Serikali Kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa Vitendo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari kwa vitendo na si kwa maneno, akisisitiza matumizi sahihi ya akili mnemba (Artificial Intelligence) kama chachu ya uwajibikaji na si kikwazo kwa waandishi wa habari.

Akizungumza jijini Arusha leo Aprili 29, 2025 wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (World Press Freedom Day 2025) ,yenye kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Uhabarishaji katika Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari”, Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa wanahabari kutumia akili mnemba kwa weledi na kuzingatia ukweli wa taarifa wanazotoa.

“Akili Mnemba itumike kama nyenzo kwa waandishi wa habari na siyo kikwazo. Mjitahidi kuitumia vizuri kwa uwajibikaji, kutoa taarifa sahihi na zenye kuzingatia maadili ya taaluma. Serikali kwa kushirikiana na Wadau tunaendelea na mchakato wa kutengeneza sera kuhusu Akili Mnemba ”, amesema Waziri Mkuu.

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Mhe. Majaliwa ametaka vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wa uwazi akihimiza utoaji wa taarifa sahihi, zinazojenga amani na mshikamano.

"2025 huu ni mwaka wa uchaguzi, sisi kama serikali, kama wadau wa uchaguzi, pindi tume huru ya uchaguzi watatoa ratiba tunatarajia nyie ndiyo mtalieleza taifa (Wanahabari) na sisi ushiriki wetu ni kuhakikisha kwamba yale yaliyo muhimu ya kuufanya uchaguzi huu kuwa wa usalama, na kila mmoja atakwenda kushiriki kwa usalama wake.. Na watu wa tume huru ya uchaguzi wametuambia kwamba uchaguzi huu watausimamia kwa uhuru na haki na uwazi. Na sisi serikali kama wadau wa uchaguzi tunataka tuwahakikishie kuwa uchaguzi huu utakuwa ni wa amani na utulivu", amesema Waziri Mkuu.

“Uchaguzi huu utakuwa wa amani na utulivu. Ninyi waandishi wa habari mtakuwa sehemu ya walinzi wa amani. Toeni taarifa zinazohamasisha kulinda tunu zetu za kitaifa,” amesisitiza.

Aidha, amevitaka vyombo vya habari kuendelea kuelimisha na kuhabarisha jamii kuhusu maendeleo ya taifa, kwa kuzingatia ukweli na uadilifu.

Waziri Mkuu ameeleza kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari kwa vitendo siyo maneno, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa taarifa na uhuru wa kujieleza.


Maelezo TV LIVE tola ARUSHA📍

🎈SIKU YA UHURU WA VYOMBO HABARI DUNIANI 2025

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger