
Na Hadija Bagasha - Tanga
Mchakato wa Uchaguzi mkuu wa chama cha waamuzi wa mpira wa miguu Tanzania (FRAT) umeanza rasmi leo April 12 ambapo wanachama wenye sifa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Mwenyekiti ngazi ya Taifa, mjumbe wa mkutano mkuu wa chama cha mpira wa miguu (TFF) , pamoja na nafasi tatu za wajumbe wa kamati ya utendaji wa chama hicho Taifa.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya chama cha waamuzi wa mpira wa miguu Tanzania (FRAT) Wakili George Banoba amewatangazia wananchama wote ambao ni waamuzi wa mpira wa miguu kwamba mchakato wa uchaguzi mkuu umeanza rasmi mapema leo ambapo fomu zitaanza kutolewa hapo kesho April 13 na kwamba zoezi hili litasitishwa April 19 mwaka huu.
"Taratibu na kanuni za kuzingatia ni kama zilivyo kwenye kanuni za chama niwaombe wananchama wote ambao wanajua wana sifa za kugombea wajitokeze na kugombea, "alisisitiza Wakili Banoba.
Wakili msomi George Banoba amesema kwamba amesema kwamba kama kuna mapingamizi taratibu nyingine zitaendelea lakini pia watafanya usaili tarehe 27 mpaka 29 April mwaka huu ambapo baadae zitaendelea taratibu nyingine za kikanuni.
"Baada ya hapo tarehe 29 tunategemea kuhitimisha zoezi la kampeni za wagombea baada ya kuwa wametangazwa kwa mchujo utakaokuwa umefanyika kwenye usaili, tunatarajia uchaguzi uhitimishwe tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa chama utakaofanyika pale jijini Tanga, "alisisitiza Wakili Banoba.
Aidha amebainisha mikakati yao kwamba kama ilivyo kwenye Katiba na kanuni ya chama ni kwamba kazi waliyopewa ni kusimamia mchakato huo wa uchaguzi na mara baada ya uchaguzi kukamilika kitakachofuata ni viongozi wapya kukabidhiwa majukumu yao na baadae kuanza kupitia mpango wa chama uliopo ambao kama wataona unafaa uendelee kutumika na iwapo utaonekana haukidhi basi utahuishwa bila kuathiri malengo ya chama.
0 comments:
Post a Comment