Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kimetangaza kufanyika kwa hafla ya utoaji tuzo za Samia Kalamu Awards tarehe 29 Aprili 2025 jijini Dodoma.Tuzo hizo zinalenga kuhamasisha uandishi wa habari za maendeleo unaogusa maisha ya wananchi na kuzingatia weledi, uchambuzi na uwajibikaji.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makundi ya tuzo ni pamoja na: tuzo za kitaifa, tuzo kwa vyombo vya habari (TV, redio, magazeti na mitandao), na tuzo za kisekta kwa waandishi walioibua mada muhimu kama afya, elimu, mazingira, jinsia na uchumi.
Hafla hiyo itarushwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili wananchi waweze kufuatilia. Waandishi na vyombo vya habari wamehimizwa kushiriki kikamilifu kuhamasisha tukio hili la kihistoria.
0 comments:
Post a Comment